
Baada ya kutumia Misoprostol, mimba inapaswa kutoka kabisa. Hata hivyo, kuna hatari ya utoaji mimba usiokamilika, ambapo baadhi ya tishu za mimba hubaki ndani ya mji wa mimba (mfuko wa kizazi). Hii inaweza kusababisha maambukizi na matatizo mengine ya kiafya.
Dalili za Utoaji mimba Usio kamili kwa kutumia misoprostol
Zifuatazo ni baadhi ya dalili za utoaji mimba usiokamili:
Kutokwa na damu kwa muda mrefu (zaidi ya wiki 2-3).
Kutokwa na damu nyingi kupita kiasi (zaidi ya kipindi cha hedhi cha kawaida, au kubadilisha pedi nyingi kwa saa chache).
Maumivu makali ya tumbo yanayoendelea kwa siku kadhaa baada ya kutumia Misoprostol.
Maumivu makali yasiyovumilika hata baada ya kutumia dawa za kupunguza maumivu.
Homa (joto la mwili kuongezeka), ambayo inaweza kuwa ishara ya maambukizi.
Kutokwa na damu bila kukoma kwa zaidi ya wiki 3.
Maumivu makali wakati unapobonyeza tumbo lako.
Nini Cha Kufanya Ikiwa Una Dalili Hizi?
Ikiwa una dalili zilizoorodheshwa hapo juu, wasiliana na daktari wako haraka kwani unahali inaohitaji matibabu ya zaidi kama vile:
Kusafisha kizazi kwa kutumia dawa.
Kufanyiwa upasuaji mdogo wa kusafisha kizazi ikiwa tishu za ujauzito hazijatoka kikamilifu.
Dawa za kutibu au kuzuia maambukizi kwenye kizazi kama kuna hatari ya maambukizi.