
PID (Pelvic Inflammatory Disease) ugonjwa unaotokana na kutotibiwa vema kwa magonjwa ya zinaa hutibiwa kwa mchanganyiko wa antibiotiki ili kuangamiza bakteria wa magonjwa ya zinaa ambao ni Neisseria gonorrhoeae, Chlamydia trachomatis, na bakteria jamii ya anaerobik. Dawa hutolewa kulingana na ukali wa dalili na matibabu hugawanywa kwenye makundi mawili yaani matibabu ya wagonjwa wa nje ya hospitali au matibabu ya wagonjwa wa ndani ya hospitalini (wanaolazwa).
Kumbuka
kabla ya kutumia dawa yoyote, wasiliana na daktari wako kabla ya kutumia dawa yoyote kuepuka madhara na usugu wa vimelea kwenye dawa. ULY CLINIC haitahusika na madhara yoyote yatakayotokea endapo hutafuata ushauri wa daktari wako.
Dawa ya PID kwa Wagonjwa wa nje (Maambukizi ya wastani au madogo)
Dawa zifuatazo hutumika katika matibabu ya wagonjwa ambao hawatarajii kulazwa hospitali kwa sababu ya PID, dawa nyingi hutumika kwa njia ya kunywa isipokuwa ceftriaxon:
Ceftriaxone
Doxycycline
Metronidazole
Matibabu mbadala ya dalili kali za PID
Cefoxitin 2g IMÂ na Probenecid 1g
Dawa za PID kwa wagonjwa wa kulazwa (Maambukizi makali)
Wagonjwa wa kulazwa hupewa dawa za kuchoma kwenye misuli au mishipa, miongoni mwa dawa hizo ni;
Ceftriaxone
Doxycycline na
Metronidazole
Matibabu mbadala wakw kwa wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya  β-lactam ni
Clindamycin na
Gentamicin IV
Tahadhari za kutumia dawa ya PID ya hospitali
Wakati wa kutumia antibiotiki za kutibu Pelvic Inflammatory Disease (PID), ni muhimu kuzingatia tahadhari zifuatazo:
Maudhi ya dawa ya PID ya hospitali
Ceftriaxone
Inaweza kusababisha mzio, maumivu kwenye sehemu ya kuchoma sindano, kuhara, au mabadiliko ya ini.
Doxycycline
Inaweza kusababisha kichefuchefu, kuhara, kuongezeka kwa hisia ya ngozi kwenye mwanga wa jua, na uharibifu wa meno kwa wajawazito na watoto chini ya miaka 8.
Metronidazole
Inaweza kusababisha kichefuchefu, ladha mbaya mdomoni, na haipaswi kutumiwa na pombe kwani inaweza kusababisha madhara makali kama vile mwitikio wa disulfiram.
Gentamicin
Inaweza kusababisha kuferi ghafla kwa figo na upotevu wa kusikia.
Uwezekano wa Mzio na mzio mkali
Wagonjwa wenye mzio na dawa jamii ya penicillin au cephalosporins wanapaswa kuwa waangalifu wanapotumia Ceftriaxone au Cefoxitin. Dalili za mzio mkali ni pamoja na uvimbe kwenye uso, kushindwa kupumua, na mshtuko wa mwili.
Matumizi sahihi ya dawa ya PID ya Hospitali
Wakati unatumia dawa hizi ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo kwa matokeo mazuri ya matibabu na kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza:
Kuhakikisha mwenza wako anapata matibabu ili kuzuia maambukizi tena.
Kuepuka kushiriki ngono hadi matibabu yatakapo kamilika.
Kufuatilia maendeleo yako ili kuhakikisha kama dalili zinapungua.
Tumia dawa zote kwa muda uliopendekezwa hata kama dalili zimepungua ili kuepuka usugu wa bakteria.
Usimeze Doxycycline kbila chakula – kula chakula ili kupunguza maudhi ya tumbo.
Epuka pombe wakati wa kutumia Metronidazole ili kuepuka maudhi makali ya dawa hii.
Rejea za mada hii:
Mediscape. Pelvic Inflammatory Disease Treatment & Management. https://emedicine.medscape.com/article/256448-treatment#:. Imechukuliwa 15.03.2025
Pelvic Inflammatory Disease CDC. (PID).https://www.cdc.gov/std/treatment-guidelines/pid.htm. Imechukuliwa 15.03.2025
ULY CLINIC. Ugonjwa wa PID. https://www.ulyclinic.com/magonjwa-na-saratani/ugonjwa-wa-pid. Imechukuliwa 15.03.2025