Doxycycline haipendekezwi kwa wajawazito, hasa baada ya wiki ya 16 ya ujauzito, kutokana na madhara yake kwa mtoto anayekua tumboni.
Madhara ya doxycycline katika ujauzito
Yafuatayo ni madhara ya doxycycline kwenye ujauzito;
Madoa ya kudumu kwenye meno na udhaifu wa enamel

Doxycycline inaweza kujikusanya kwenye meno ya mtoto tumboni na kusababisha madoa ya njano-kahawia ya kudumu na matatizo ya meno.
Kuchelewesha ukuaji wa mifupa
Dawa hii hujifunga na madini ya kalsiamu kwenye mifupa ya kijusi, hali inayoweza kuchelewesha ukuaji wa mifupa.
Sumu kwa ini la mama
Ingawa ni nadra kutokea, doxycycline inaweza kusababisha uharibifu wa ini kwa wajawazito.
Hofu ya matatizo ya kimaumbile kwa mtoto (sumu kwenye uumbaji wa kijusi)
Hakuna ushahidi mkubwa unaoonyesha kuwa doxycycline husababisha kasoro kubwa za kimaumbile kwa binadamu, lakini kwa kuwa inaathiri meno na mifupa, inashauriwa kuepukwa.
Je, wakati gani doxycycline inaweza kutumika?
Hali na magonjwa yafuatayo yanaweza lazimu daktari akuandikie utumie kwa kuwa inafaida kuliko madhara yake;
Katika kipindi cha kwanza cha ujauzito , doxycycline inaweza kutumika ikiwa hakuna dawa salama mbadala na faida yake inazidi hatari zake zinazoweza kutokea
Katika magonjwa hatari kama Rocky Mountain Spotted Fever, Homa Q, au leptospirosis kali.
Wataalamu wengine wanaamini kuwa matumizi ya muda mfupi (<2 wiki) katika kipindi cha kwanza cha ujauzito yanaweza kuwa salama kiasi.
Mbadala salama wa doxycycline
Kulingana na aina ya maambukizi, dawa salama zaidi ni:
Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI): Amoxicillin, Nitrofurantoin (epuka baada ya wiki ya 36)
Maambukizi ya njia ya hewa: Azithromycin, Amoxicillin-Clavulanate
Uzuiaji wa Malaria: Clindamycin (ikiwa ni lazima)
Maambukizi ya Klamidia: Azithromycin
Hitimisho
Doxycycline inapaswa kuepukwa baada ya wiki ya 16 ya ujauzito, isipokuwa pale inapokuwa muhimu sana kuliko madhara yanayoweza kutokea kwa mama. Ni vyema kuchagua dawa mbadala zinazojulikana kuwa salama kwa mama na mtoto.
Rejea za mada hii
Nahum GG, Uhl K, Kennedy DL. Antibiotic use in pregnancy and lactation: What is and is not known about teratogenic and toxic risks. Obstet Gynecol. 2006;107(5):1120-38.
FDA. Doxycycline use in pregnant and lactating women. U.S. Food and Drug Administration; 2018 [cited 2025 Apr 4]. Available from: https://www.fda.gov
Cross R, Ling C. Safety of doxycycline use in pregnancy: A review. Am J Perinatol. 2021;38(8):798-805.
Todd SR, Dahlgren FS, Traeger MS, Beltrán-Aguilar ED, Marianos DW, Hamilton C, et al. No visible dental staining in children treated with doxycycline for suspected Rocky Mountain spotted fever. J Pediatr. 2015;166(5):1246-51.
Kazy Z, Puhó EH, Czeizel AE. Teratogenic potential of doxycycline treatment during pregnancy: A population-based case-control study. Congenit Anom (Kyoto). 2007;47(5):2-8.
Rubinstein E. History of tetracycline use and resistance. J Antimicrob Chemother. 2003;51(Suppl 1):i5-i7.