Katika makala hii utajifunza kuhusu magonjwa inayotibu, maudhi, wakati gani wa kumwona daktari, usugu wa vimelea kwenye dawa na tahadhari kabla ya kutumia dawa erythromycin.

Erythromycin inatibu nini?
Erythromycin ni dawa jamii ya antibiotiki iliyopo kwenye kundi macrolide na hutumika kutibu maambukizi mbalimbali ya bakteria, ambayo yameorosheshwa hapa chini;
Maambukizi ya Njia ya Hewa
Hutibu magonjwa kama nimonia, bronkaitisi, kikohozi kikuu (Bordetella pertussis).
Maambukizi ya Ngozi na Tishu Laini
Hutibu chunusi, maambukizi kwenye ngozi na majipu kwenye vinyweleo(impetigo)
Magonjwa ya Zinaa
Hutibu kaswende, klamidia (kwa wagonjwa wenye mzio wa penicillin)
Maambukizi ya Macho
Hutibu maambukizi kwenye macho kwa watoto wachanga kutokana na bakteria Neisseria gonorrhoeae kwenye sehemu ambako hakuna usugu wa kimelea kwenye dawa hii.
Maambukizi ya Tumbo na MatumboÂ
Huua kimelea Helicobacter pylori hivyo huweza kuwa kutumika pamoja na dawa zingine kwenye matibabu ya vidonda vya tumbo.
Kinga Dhidi ya Diphtheria na Kikohozi Kikuu
Hutumika kuzuia maambukizi kwa walio hatarini.
Dawa mbadala kwa Wenye Mzio wa Penicillin
Hutumika kutibu magonjwa yanayotinika kwa dawa jamii ya penicillin endapo hazipo salama kutumika.
Maudhi ya erythromycin
Sehemu hii imegawa maudhi katika makundi mawili, maudhi ya kawaida na maudhi makali ambayo hufahamika pia kama madhara. Baadhi ya maudhi ya erythromycin yanayoripotiwa sana yameorodheshwa hapa chini;
Maudhi ya kawaida ya Erythromycin
Maudhi ya kawaida yanayotokea sana kutokana na kutumia erythromycin ni pamoja na;
Kichefuchefu na kutapika.
Maumivu ya tumbo na kuharisha
Kukosa hamu ya kula
Upele au kuwashwa kwa ngozi
Kupungua kwa usikivu wa muda (nadra, kwa dozi kubwa)
Maudhi makali ya dawa
Maudhi makali(madhara) ya dawa yanayotokea sana kutokana na kutumia erythromycin ni pamoja na;
Mzio Mkali (Mzio wa anafailaksis) – kuvimba, kushindwa kupumua.
Mapigo ya Moyo yasiyo ya kawaida (Kuongezeka kwa na arizmia) – huweza kusababisha matatizo ya moyo.
Madhara kwa Ini (husabaisha hepatitis ya kikolestatik) – manjano ya ngozi na macho, maumivu ya juu ya tumbo.
Maambukizi makali ya matumbo (kutona na kuzaliana kwa C. difficile) – huonekana na dalili ya kuharisha kali, hatari ya colitis.
Kupungua kwa usikivu – mara chache sana hutokea, hali inaweza kuwa ya kudumu kwa kama imetumika dozi kubwa au dozi ya muda mrefu.
Usugu wa vimelea kwenye Erythromycin
Usugu wa bakteria unaongezeka duniani kote, hasa katika:
Maambukizi ya njia ya hewa: Yanayosababishwa na kimelea Streptococcus pneumoniae na Haemophilus influenzae zinaonyesha usugu mkubwa.
Magonjwa ya Zinaa (STIs):Â Yanayosababishwa na Neisseria gonorrhoeae. bakteria huyu ana usugu wa hali ya juu kwenye dawa hii katika baadhi ya maeneo.
Maambukizi ya tumbo na matumbo: Helicobacter pylori ana usugu wa wastani hadi wa hali ya juu, hivyo haipaswi kutumika katika tiba ya vidonda vya tumbo.
Wakati gani wa kumwona daktari ukiwa unatumia Erythromycin?
Tafuta msaada wa matibabu haraka ikiwa unapata hali na dalili zifuatazo baada ya kuanza kutumia erythromycin kwa mdaada wa haraka;
Mzio mkali – huambatana na kuvimba koo, njia ya hewa, kushindwa kupumua, upele au harara kali.
Hali kali ya kuharisha (kuharisha damu au kuharisha kwa zaidi ya siku 3) – huweza kuwa dalili za maambukizi makali ya matumbo.
Mapigo ya moyo yasiyo kawaida au mpapatiko wa moyo – inaonyesha kuna hatari ya matatizo makubwa ya moyo.
Manjano ya ngozi au macho – huashiria kuna tatizo katika ini.
Kichefuchefu, kutapika mara kwa mara, au maumivu makali ya tumbo – dalili hii huashiria usumu wa dawa mwilini.
Kupungua kwa usikivu au kelele masikioni (tinitaz) – hasa kwa aliyetumia dozi kubwa au dozi ya muda mrefu.
Hali na magonjwa mbalimbali ambayo yanafanya dawa Erythromycin isitumike
Hali ya magonjwa yafuatayo yanalazimu dawa erythromycin isitumike, hivyo mbadala wake unabidi kutafutwa na daktari wako. Hali hizo ni pamoja na;
Matatizo ya Moyo (Ongezeko la QT, Arizimia) – kwa wagonjwa wa aina hii, kutumia erythromycin kunaweza kuongeza matatizo ya moyo.
Magonjwa ya Ini – kuna hatari kubwa ya usumu kwenye ini.
Mayathenia Gravis – Kutumia erythromycine kunaweza kuzidisha udhaifu wa misuli.
Ujauzito na unyonyeshaji – kwa ujumla ni salama lakini inapaswa kutumiwa kwa usimamizi wa daktari.
Mwingiliano na dawa nyingine – huweza kuwa na madhara makubwa inapochanganywa na dawa kundi la statin, dawa za kuyeyusha damu, na baadhi ya dawa za arizimia.
Hitimisho
Erythromycin ni antibiotiki muhimu kwa matibabu ya maambukizi mbalimbali, hata hivyo inapaswa kutumiwa kwa tahadhari kutokana kuweza kusababisha athari kwenye moyo, ini, na usugu wa bakteria kwenye dawa.
Rejea za mada hii
Marchant JM, et al. Antibiotics for prolonged wet cough in children. Cochrane Database Syst Rev. 2018 Jul 31;7(7):CD004822.
Amsden GW. Erythromycin, clarithromycin, and azithromycin: are the differences real? Clin Ther. 1996 Jan-Feb;18(1):56-72; discussion 55.
Schmidt N, et al. Tretinoin: A Review of Its Anti-inflammatory Properties in the Treatment of Acne. J Clin Aesthet Dermatol. 2011 Nov;4(11):22-9.
Morgan JA, et al. StatPearls [Internet]. StatPearls Publishing; Treasure Island (FL): Aug 11, 2024. Group B Streptococcus and Pregnancy.
Camilleri M, et al., American College of Gastroenterology. Clinical guideline: management of gastroparesis. Am J Gastroenterol. 2013 Jan;108(1):18-37; quiz 38.
Tenson T, et al. The mechanism of action of macrolides, lincosamides and streptogramin B reveals the nascent peptide exit path in the ribosome. J Mol Biol. 2003 Jul 25;330(5):1005-14.
Liang JH, et al. Structure-activity relationships and mechanism of action of macrolides derived from erythromycin as antibacterial agents. Curr Top Med Chem. 2013;13(24):3131-64.
Maekawa T, et al. Erythromycin inhibits neutrophilic inflammation and mucosal disease by upregulating DEL-1. JCI Insight. 2020 Aug 06;5(15)
Guo MT, et al. Insights into the amplification of bacterial resistance to erythromycin in activated sludge. Chemosphere. 2015 Oct;136:79-85.
Varaldo PE, Montanari MP, Giovanetti E. Genetic elements responsible for erythromycin resistance in streptococci. Antimicrob Agents Chemother. 2009 Feb;53(2):343-53.