
Tangawizi na kitunguu saumu ni mimea yenye thamani kubwa kiafya ambayo hutumiwa kwa madhumuni mbalimbali ya tiba. Kwa wanaume, vyakula hivi vinaweza kuwa na manufaa makubwa kwa afya ya uzazi, nguvu za mwili, na kinga ya mwili.
Zifuatazo ni faida za tangawizi na kitunguu saumu kwa mwanaume;
Kuimarisha nguvu za kiume na afya ya uzazi
Tangawizi husaidia kuongeza mzunguko wa damu, ikiwemo kwenye uume, hivyo kusaidia kudumisha nguvu za kiume na kupunguza tatizo la kushindwa kusimamisha, wakati huo kitunguu saumu kina viambata vinavyosaidia kuongeza uzalishaji wa manii (mbegu za kiume) na kuboresha ubora wake.
Kuboresha mzunguko wa damu
Viinilishe vya tangawizi kama gingerol husaidia kupunguza msongamano wa damu kwenye mishipa ya damu hivyo kuimarisha mtiririko wake wakati huo kitunguu saumu kina allicin, ambacho husaidia kupunguza shinikizo la damu na hatari ya kupata magonjwa ya moyo.
Kuongeza nguvu na nguvu za mwili
Tangawizi huchochea umetaboli wa mwili, huongeza nishati, na kupunguza uchovu wa mwili, wakati huo kitunguu saumu kina uwezo wa kupunguza uchovu na kuongeza nguvu za mwili kwa wanaofanya kazi ngumu au mazoezi.
Kupunguza mafuta mwilini na kitambi
Tangawizi husaidia kuchoma mafuta haraka na kupunguza unene wa tumbo, jambo linalohusiana na afya bora ya uzazi kwa wanaume wakati huo kitunguu saumu husaidia kupunguza mafuta mabaya mwilini (Lehemu ya LDL) na hivyo kuboresha afya ya moyo.
Kuimarisha kinga ya mwili
Tangawizi ina viuajisumu vinavyosaidia mwili kupambana na magonjwa na kuongeza kinga dhidi ya maambukizi wakati huo kitunguu saumu kina viuajivimelea vya asili ambavyo husaidia kupambana na bakteria, virusi, na fangasi.
Kupunguza msongo wa mawazo na kuuimarisha mwili
Tangawizi ina uwezo wa kupunguza msongo wa mawazo na kuboresha hali ya kisaikolojia, ambayo ni muhimu kwa afya ya uzazi wakati kitunguu saumu husaidia kuboresha usingizi na kupunguza uchovu wa mwili na akili.
Madhara ya kutumia tangawizi na kitunguu saumu nyingi kupita kiasi
Kila kitu kisipotumiwa kwa kiwango kinachohitajika huwa na madhara mwilini, yafuatayo ni madhara ya kutumia viungo hivi kwa wingi;
Tatizo la tumbo na kiungulia
Matumizi makubwa ya tangawizi yanaweza kusababisha kiungulia, maumivu ya tumbo, au kuhisi kichefuchefu.Wakati kitunguu saumu kikiliwa kwa wingi kinaweza kusababisha gesi tumboni na kuharisha.
Kupunguza shinikizo la damu kupita kiasi
Tangawizi na kitunguu saumu vina uwezo wa kushusha shinikizo la damu, hivyo kwa watu wenye shinikizo la chini, vinaweza kusababisha kizunguzungu na udhaifu.
Kuongeza hatari ya kutokwa na damu kupita kiasi
Kitunguu saumu na tangawizi vina uwezo wa kufanya damu isiwe nzito (kupunguza ugandaji wa damu), hivyo matumizi mengi yanaweza kuongeza hatari ya kutokwa na damu kwa urahisi, hasa kwa watu wanaotumia dawa za kuzuia damu kuganda.
Kuathiri harufu ya mwili na pumzi
Kitunguu saumu kikiliwa kwa wingi kinaweza kusababisha harufu mbaya ya mwili na pumzi, jambo linaloweza kuwa kero kwa wengine.
Matatizo ya figo na ini
Matumizi ya muda mrefu na kwa wingi yanaweza kuathiri afya ya figo na ini kwa watu wenye matatizo ya viungo hivi.
Â
Jinsi ya kutumia tangawizi na kitunguu saumu kupata faida zake
Kunywa chai ya tangawizi kila siku asubuhi ili kuboresha mzunguko wa damu.
Tafuna kitunguu saumu kibichi au changanya na asali kwa ajili ya kuimarisha afya ya uzazi.
Tengeneza sharubati ya tangawizi na kitunguu saumu kwa kuchanganya vyote na maji ya limau.Ongeza kwenye chakula kama viungo vya kawaida kwa ladha na manufaa zaidi.
Tahadhari
Epuka kutumia kwa wingi kwani vinaweza kusababisha matatizo ya tumbo kwa baadhi ya watu.
Rejea za mada hii
Â
Afzal M, et al.. Ginger: An ethnomedical, chemical and pharmacological review. Drug Metabol Drug Interact. 2001;18(3-4):159–90.
Aeschbach R, et al. Antioxidant actions of thymol, carvacrol, [6]-gingerol, zingerone and hydroxytyrosol. Food Chem Toxicol. 1994;32(1):31–6.
Aggarwal B. et al.. Potential of spice-derived phytochemicals for cancer prevention. Planta Med. 2008;74(13):1560–9.
Ahmad N, et al.. Antioxidants in chemoprevention of skin cancer. Curr Probl Dermatol. 2001;29:128–39.
Ahmed R. S, et al.. Influence of dietary ginger (Zingiber officinales Rosc.) on antioxidant defense system in rat: Comparison with ascorbic acid. Indian J Exp Biol. 2000;38(6):604–6.
Ahmed R. S, et al. Influence of dietary ginger (Zingiber officinales Rosc.) on oxidative stress induced by malathion in rats. Food Chem Toxicol. 2000;38(5):443–50.
Ahmed R. S, et al.. Protective effects of dietary ginger (Zingiber officinales Rosc.) on lindane-induced oxidative stress in rats. Phytother Res. 2008;22(7):902–6.
Jiang T.A. Health Benefits of Culinary Herbs and Spices. J. AOAC Int. 2019;102:395–411. doi: 10.5740/jaoacint.18-0418.Â
Petrovska B.B., Cekovska S. Extracts from the history and medical properties of garlic. Pharmacogn. Rev. 2010;4:106–110. doi: 10.4103/0973-7847.65321.Â
Setiawan V.W, et al. Allium vegetables and stomach cancer risk in China. Asian Pac. J. Cancer Prev. APJCP. 2005;6:387–395.
Diretto G., et al. Tissue-specific accumulation of sulfur compounds and saponins in different parts of garlic cloves from purple and white ecotypes. Molecules. 2017;22:1359. doi: 10.3390/molecules22081359.
5.Gorinstein S., et al. Comparison of the main bioactive compounds and antioxidant activities in garlic and white and red onions after treatment protocols. J. Agric. Food Chem. 2008;56:4418–4426. doi: 10.1021/jf800038h.Â