Swali 1: Je ni kawaida kwa mtoto mchanga kupata choo mara kwa mara kidogo kidogo?
Jibu:
Kujisaidia ni afya kwa kichanga na husaidia kuondoa maumivu ya tumbo(chango) hivyo hakuna shida na pia itapungua siku zinavyoenda.
Swali 2: Kinachonifanya nipate hofu ni kuna muda nakuta amejisaidia majimaji tu kaloana sehemu ya haja kubwa, hii ni kawaida?
Jibu:
Majimaji kuzunguka njia ya haja kubwa yanaweza kutokana na mkojo wa mtoto haswa akiwa amevalishwa nepi au pampasi isiyofyonza maji vema. Kwa kuwa mara nyingi mtoto hulala chali, anapokojoa ni rahisi mkojo wake kwenda katikati ya makalio na mapaja na hivyo ukaona dalili kama hiyo.
Swali 3: Je ni kawaida kichanga wa mwezi mmoja kwenda haja kubwa mara tisa kwa siku?
Ndio, Ni kawaida kwa kichanga kwenda haja kubwa mara 9 au zaidi katika kipindi cha masaa 24 hasa endapo kinyesi kinaonekana kimetengenezwa vema, hakina harufu isiyo ya kawaida na mtoto hana dalili za hatari( Soma kuhusu dalil za hatari kwa kubofya hapa)
Soma zaidi kuhusu haja kubwa kwa mtoto chini ya miezi 3 kwa kubofya hapa