Swali:
Inawezekana kutokwa na damu nying na ya mabonge bila maumivu yoyote na mimba kuendelea kuwepo?
Jibu:
Ndio inawezekana.
Kutokwa damu ya mabonge baada ya kutumia dawa ya kutoa mimba inaweza maanisha mimba imetoka au la. Mara nyingi mimba ikitoka damu yake huwa ngingi na kuambatana na maumivu ya tumbo yanayoweza kuwa ya kawaida au makali. Damu inayotoka huambatana na tishu za ujauzito au viungo vya mwili wa mtoto na hivi hutegemea mimba ilikuwa na umri gani.
Maelezo zaidi:
Njia pekee ya kufahamu mimba imetoka ni kwa kufanya kipimo cha ujauzito ambacho mqjibu yake huwa sahihi angalau wiki la pili toka imetoka. Hii ni kwa sababu katika kioindi hiki, kiwango cha homoni ya jauzito(HCG) kwenye mkojo huwa kidogo kuweza kutambuliwa na kipimo.
Njia nyingine ya haraka inayoweza kutumika ni kwa kutumia kipimo cha picha ya sauti ya kizazi(ultrasound). Kipimo hiki hutambua kama tishu za mimba zimeshatoka kwenye kuta za mji wa mimba au la. Licha ya kuwa kipimo kizuri kutambua mapema kuwa mimba imetoka au la, majibu ya kipimo hutegemea uwezo na uzoefu wa mpigaji wa picha kupiga na kutafsiri picha hiyo. Wapi unaweza kupata maelezo zaidi? Soma zaidi kwenye makala nyingine kuhusu kutoa mimba kwa dawa katika tovuti hii.