
Ndio, baadhi ya dawa za kufubaza VVU zinaweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume, hata hivyo tatizo hili halitokei kwa kila mtu.
Upungufu wa nguvu za kiume kwa mtu anayetumia ARVs husababishwa na mambo yafuatayo.
Madhara ya dawa
Baadhi ya dawa za ARV huathiri kiwango cha homoni testosterone, mzunguko wa damu, au mfumo wa neva za fahamu hivyo kusababisha matatizo ya nguvu za kiume.
Dawa zifuatazo zinathibitishwa kusababisha upungufu wa nguvu za kiume;
Efavirenzi- husababisha mfadhaiko na wasiwasi
Dawa katika kundi la protease inhibitors kama vile atazanavir na lopinavir- huathiri viwango vya homoni testosterone ambayo ni muhimu sana kwa nguvu za kiume.
Zidovudine- husababisha uchovu and na kupungua kwa stamina
Athari za VVU
VVU huathiri nguvu za kiume kwa njia zifuatazo;
Huathiri mishipa ya damu hivyo kupunguza mzunguko wa damu kwenye uume.
Hupunguza kiwango cha homoni testosterone.
Huleta mfadhaiko na msongo
Visababishi vingine
Mara nyingi watu wanaotumia ARVs huwa na changamoto nyingine za kiafya zinazoweza kuathiri nguvu za kiume mfano kisukari, shinikizo la juu la damu, sonona na msongo wa mawazo.
Hitimisho
Ni Dhahiri kwamba kuna uhusiano kati ya matumizi ya dawa za ARV na afya ya uzazi ya wanaume. Hata hivyo dawa hizi ni muhimu katika kudhibiti virusi vya ukimwi (HIV) na kupunguza kiwango cha maambukizi mapya.
Wasiliana na daktari wako endapo unaona mabadiliko katika suala zima la afya ya uzazi.
Rejea za mada hii
Pilatz A, Discher T, Lochnit G, et al. “Semen quality in HIV patients under stable antiretroviral therapy is impaired compared to WHO reference values and on sperm proteome level.” AIDS 2014; 28: 875–80.
Frapsauce C, Grabar S, Leruez-Ville M, et al. “Impaired sperm motility in HIV-infected men: an unexpected adverse effect of efavirenz?” Hum Reprod 2015; 30:1797–806.
Dulioust E, Du Al, Costagliola D, et al. “Semen alterations in HIV-1 infected men.” Hum Reprod 2002;17:2112–18.