Mtu ambaye ni mwathirika wa HIV lakini anayetumia ARV kwa ufasaha na CD4 zakezipo vizuri au kuwa kwa kiwango cha juu.
Ni kweli akipma HIV/AIDS kwa kutumia kitepe cha "SD Biolline au "UNIGOLD majibu yanaweza kuwa NEGATIVE?? yaan asionekane kuwa ni mgonjwa kupitia ivyo vipimo??
Virusi vya UKIMWI -VVU (HIV) husababisha mwili kutengeneza protini mbalimbali ambazo ni walinzi wa mwili, protini hizi huitwa kwa jina la antibodies. Antibodies zilizotengenezwa hupambana ili kuondoa maambukizi ya virusi kwenye damu. Hata hivyo maambukizi yakiisha au yasiishe antibody za HIV zitaendelea kuwepo kwenye damu ili tu maambukizi mengineya kirusi yakiingai kwenye damu, mara moja walinzi hao wataanzisha shambulio dhidi ya yao. Kumbuka kila maambukizi hutengeneza antiboy inayoendana na maambukizi hayo.
Antibodies za HIV huwa hazipotei kwenye damu mwilini zikishatengenezwa na hivyo licha ya kutumia dawa ipasavyo mwathirika lazima aendelee kuwa HIV positive kwa hiki kipimo Cha HIV SD bioline.
Kwa maswali mengine uliza na ujibiwe kupitia email au forumu hii