Kucheua tindikali ( acid kupanda kooni) ni ugonjwa unaotokea sana. Baadhi ya watu hata hivyo hupata tatizo la tumbo kujaa, kubeua mara kadhaa baada ya kula.
Chakula huchukua nafasi kubwa katika matibabu ya hali hizi pamoja na ugonjwa wa kucheua tindikali.
Makala hii imeelezea kuhusu vyakula vinavyochochea au kusababisha kucheua tindikali na kiungulia na vile ambavyo vinapunguza au kutibu tatizo hili.
Vyakula vinavyosababisha kiungulia/kucheua tindikali
Vyakula hivi hufahamika kulegeza koki ya chini ya umio na hivyo kusababisha kucheua na matatizo mengine ya tumbo;
Vyakula vya kukaanga
Piza
Chipsi jna vitafunwwa vingine vyenye mafuta kwa wingi
Pilipili na chili sosi
Nyama yenye mafuta pamoja na soseji
Siagi
Sosi ya njanya
Nyanya
Matunda jamii ya citrus kama limao, ndimu
Siki ya tufaa
Chocolate
Minti hupatikana kwenye bazoka (bablishi) na baadhi ya dawa ya mswaki n.k
Vinywaji vilivyotiwa carbon kama vile soda n.k
Nanasi
Machungwa
Vyakula vyenye viungo kwa wingi kama vitunguu, tangawizi na pilipili
Kahawa
Pombe
Vyakula vinavyozuia kiungulia na kucheua tindikali
Kuna aina kadhaa ya makundi ya vyakula vinavyozuia kiungulia, vyakula hivi huwa na ualkali kwa wingi. Baadhi yake ni;
Nafaka zisizokobolewa kama mchele wa brauni, mtama na uwele
Vyakula jamii ya mizizi kama vile viazi vitamu, karoti na kiazi kitamu (biti)
Mboga za majani kama vile asparagazi, brokoli na maharagwe ya kijani au saladi yenye mbogha za majani kwa wingi
Ndizi
Boga
Karanga
Funnel
Ute wa yai
Tango
Tikiti maji
Chai yenye tangawizi kwa kiasi kidogo
Spinachi
Maziwa ya mgando yenye mafuta kidogo
Nyama isiyo na mafuta
Mambo mengine ya kuzingatia
Epuka kula mlo mzito, kula milo midogo midogo ili kuzuia tumbo kujaa na kulegea kwa koki inayozuia kucheua chakula.
Epuka kula unapokaribia wakati wa kulala haswa ndani ya masaa 3 hadi 4 kabla ya kulala
Tumia dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali kama utakavyoshauriwa na daktari wako
Kuwa na uzito wa kiafya
Acha kutumia pombe
Acha kuvuta sigara
Usile haraka haraka
Kaa wima angalau masaa mawili baada ya kula
Usivae nguo za kubana
Tumia mto wakati wa kulala kufanya kichwa kiwe juu kidogo ili kuzuia kucheua
Rejea za mada hii;
John hopkins medicine. GERD Diet: Foods That Help with Acid Reflux (Heartburn). https://www.hopkinsmedicine.org/health/wellness-and-prevention/gerd-diet-foods-that-help-with-acid-reflux-heartburn
Acid reflux (GER and GERD) in adults. (n.d.). niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/acid-reflux-ger-gerd-adults
Allergens and allergic asthma. (2015). aafa.org/page/allergic-asthma.aspx
Diet changes for GERD. (2021). aboutgerd.org/diet-lifestyle-changes/diet-changes-for-gerd.html
Kahrilas P, et al. (2017). Emerging dilemmas in the diagnosis and management of gastroesophageal reflux disease. 10.12688/f1000research.11918.1
Kaur K, et al. (2015). Chapter 6: Medicinal benefits of ginger in various gastrointestinal ailments: Use in geriatric conditions. sciencedirect.com/science/article/pii/B9780124186804000063
Morozov, S, et al. (2018). Fiber-enriched diet helps to control symptoms and improves esophageal motility in patients with non-erosive gastroesophageal reflux disease. ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5989243/