
Levonorgestrel (kiambato kikuu cha P2) hufanya kazi ndani ya masaa 24 hadi 48 baada ya kumezwa, lakini ufanisi wake hupungua kadri muda unavyopita.
Tafiti zinaonyesha kuwa P2 inaweza kuchelewesha uovuleshaji kwa wastani wa siku 5, lakini hii inategemea hatua ya mzunguko wa hedhi ya mtu.
Namna P2 inavyofanya kazi kwa muda
Ikiwa imechukuliwa kabla ya Uovuleshaji:
Inaweza kuzuia yai lisitoke kwa kuchelewesha uovuleshaji.
Ufanisi wake ni mzuri zaidi ikiwa imechukuliwa haraka (ndani ya masaa 12-24 baada ya ngono isiyo salama).
Ikiwa uovuleshaji tayari umetokea:
P2 haitafanya kazi vizuri kama yai limeshatolewa na mbegu zinaweza kulifikia.
P2 haitazuia mbegu kuchavusha yai ikiwa tayari limeshatolewa kwenye ovari.
Ufanisi wa P2 kutegemea muda wa matumizi
Ukimeza ndani ya masaa 24 inazuia kwa asilimia 95
Ukimeza ndani ya masaa 48 inazuia kwa asilimia 85
Ukimeza ndani ya masaa 72 inazuia kwa asilimia 58
Muda bora wa kutumia P2 ni mapema iwezekanavyo, kwa sababu kadri muda unavyopita, uwezo wake wa kuzuia mimba hupungua.
Hitimisho Muhimu
P2 hufanya kazi ndani ya masaa 24-48 kwa kuchelewesha Upvuleshaji.
Ikiwa tayari uovuleshaji umetokea, P2 haina ufanisi mkubwa.
Njia bora za kuzuia mimba kwa uhakika ni njia za kudumu kama vidonge vya kila siku, sindano, au vijiti.