
Ikiwa umeshauriwa na mtoa huduma wa afya kutumia Misoprostol kwa njia ya uke, fuata hatua hizi kwa usahihi ili kuongeza ufanisi wake na kupunguza madhara:
Hatua za Kufuata Kuweka Misoprostol Ukeni kwa Utoaji wa Mimba
Andaa Mazingira
Nawa mikono yako kwa sabuni na maji safi.
Hakikisha unakuwa katika mazingira safi na tulivu.
Unaweza kuvaa glavu safi (si lazima, lakini ni bora kwa usafi).
Kuweka Misoprostol Ukeni
Lala chali (mgongo chini) au kaa na kupanua miguu ili kupata nafasi nzuri.
Tumia kidole kusukuma vidonge 3 hadi 4 vya Misoprostol (kila kimoja 200 mcg) ndani kabisa ya uke.
Hakikisha vidonge vinakaa juu karibu na shingo ya kizazi (cervix) kwa matokeo bora.
Baada ya kuweka vidonge, laza mwili kwa dakika 30 ili kuzuia vidonge kuteleza nje.
Baada ya Kuweka vidonge vya Misoprostol ukeni utegemee nini?
Dalili kama maumivu ya tumbo, kuharisha, kuvuja damu nyingi, na kuhisi baridi zinaweza kuanza ndani ya masaa 1-4.
Damu inaweza kutoka kwa siku 7-14, lakini kawaida hutulia baada ya siku chache.
Usitumie pedi za kuingiza ukeni (tamponi), badala yake tumia pedi ili kufuatilia kiwango cha damu kinachotoka.
Epuka kufanya ngono hadi damu itakapokoma kabisa ili kuzuia maambukizi.
Wakati gani unapaswa Kuwasiliana na Daktari haraka ikiwa umetumia misoprostol?
Damu inaendelea kutoka kwa zaidi ya wiki 2 kwa kiasi kikubwa sana.
Unapata homa kali (zaidi ya 38°C) au harufu mbaya kutoka ukeni (huenda kuna maambukizi).
Unapata maumivu makali yasiyopungua hata baada ya kutumia dawa za maumivu.
Hakuna damu yoyote inayotoka ndani ya masaa 24 baada ya kutumia Misoprostol (inaweza kuwa ishara ya utoaji mimba usiofanikiwa).
Wapi utapata maelezo zaidi?
Soma kuhusu kutokwa damu baad aya kuweka misoprostol ukeni katika makala ya siku za kutoka damu baada ya kutumia misoprostol.
Rejea za mada hii:
NCBI. Misoprostol. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK539873/. Imechukuliwa 15.03.2025
Schaff EA, et al. Vaginal misoprostol administered at home after mifepristone (RU486) for abortion. J Fam Pract. 1997 Apr;44(4):353-60. PMID: 9108832.
Allen R, et al. Uses of misoprostol in obstetrics and gynecology. Rev Obstet Gynecol. 2009 Summer;2(3):159-68. PMID: 19826573; PMCID: PMC2760893.
Carbonell JL, et al. Oral and vaginal misoprostol 800 microg every 8 h for early abortion. Contraception. 2003 Jun;67(6):457-62. doi: 10.1016/s0010-7824(03)00043-x. PMID: 12814814.