Usomaji wa majibu ya kipimo cha ukimwi huweza kuwa ya aina tatu. Majibu chanya au HIV positive, Majibu Hasi au HIV negative na majibu ya tatanishi. Makala hii inazungumzia kuhusu Majibu chanya ya kipimo cha UKIMWI
Kipimo cha ukimwi kuwa positive humaanisha kuwa una dalili ya maambukizi kwenye damu na unapaswa kufanya vipimo zaidi kuthibitisha uwepo wa VVU isipokuwa kama umefanya kipimo cha uwepo wa vinasababa vya VVU.
Je, kuna visababishi vingine vinavyopelekea majibu ya kipimo cha UKIMWI kuwa positive?
Mbali na maambukizi ya VVU, kuna visababishi vingine vinavyoweza kupelekea kupata majibu chanya ya kipimo cha UKIMWI ambavyo ni:
Maambukizo ya magonjwa mengine kama Kirusi cha Epistein-Bar na ugonjwa wa Malaria, babesiosis
Matatizo ya kiufundi endapo kipimo hakijafanyika kwa usahihi au damu kuchanganyika na ya mtu mwingine mwenye VVU
Kuwa na baadhi ya magonjwa ya kujitafuta kwa mfumo wa kinga mwilini kama ugonjwa wa lupasi
Kupata chanjo aina fulani hivi karibuni
Hali na magonjwa mengine ya mwili kama vile kuwa na kiwango cha juu cha kemikali bilirubin kwenye damu.
Je nifanyaje kama majibu ya kipimo cha ukimwi ni positive?
Endapo utajipima nyumbani kwa kipimo cha HIV na kikawa positive, wasiliana na daktari wako mara moja kwa ushauri na tiba. Daktari wako atarudia kipimo na kufanya kipimo kingine cha kuthibitisha uwepo wa maambukizi kabla ya kukushauri kutumia dawa kama vipimo vitathibitisha kuwa una maambukizi ya VVU.
Picha ya majibu ya kipimo cha Virusi vya ukimwi
Kwa mada ya picha ya kusoma majibu ya ukimwi ingia kwenye makala ya majibu 7 ya kipimo cha Kirusi cha UKIMWI. Na ikiwa majibu ya kipimo chako yamebadilika kuwa positive baada ya kusoma baada ya masaa machache kupita, soma katika makala ya kubadilika kwa majibu ya kipimo cha ukimwi.
Rejea za mada hii
Yusuke Ainoda, et al. False-positive fourth-generation HIV test result in a woman with Plasmodium malariae malaria, Transactions of The Royal Society of Tropical Medicine and Hygiene, Volume 117, Issue 2, February 2023, Pages 147–148,https://doi.org/10.1093/trstmh/trac098. Imechukuliwa 13.11.2024
He JZ, et al. Acute Babesiosis Causing a False-Positive HIV Result: An Unexpected Association. Case Rep Infect Dis. 2023 Jul 24;2023:6271710. doi: 10.1155/2023/6271710. PMID: 37528903; PMCID: PMC10390267.Imechukuliwa 13.11.2024
False positive results on HIV tests. https://www.aidsmap.com/about-hiv/false-positive-results-hiv-tests. Imechukuliwa 13.11.2024