Swali la mssingi
Doctor, naomba kufahamu kama kitanzi kinaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa kwenye kizazi, na kama ndio, nn afanye mtu anaetumia njia hii ili asipate maambukizi ya magonjwa kwenye via vya uzazi?
Majibu

Ndiyo, kitanzi, kama njia ya uzazi wa mpango, kinaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi kwenye via vya uzazi, hasa mwanzoni baada ya kufungwa. Lakini si kwamba kitanzi chenyewe kinaambukiza, bali hali ya mazingira ya uke na namna kinavyowekwa inaweza kuchangia kupata maambukizi.
Maambukizi gani yanaweza kutokea?
Maambukizi ya via vya ndani vya uzazi (PID ) yanaweza kutokea ikiwa:
Kitanzi kimewekwa wakati tayari kulikuwa na maambukizi kwenye uke au mlango wa kizazi.
Usafi haukuzingatiwa wakati wa kuweka kitanzi.
Mtu ana wapenzi wengi bila kutumia kondomu — huongeza hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama vile klamydia au gono.
Dalili za maambukizi kwenye via vya uzazi
Ukiona dalili zifuatazo hakikisha unawasiliana na daktari kwa uchunguzi na tiba;
Maumivu ya tumbo la chini
Kutokwa na uchafu usio wa kawaida ukeni
Homa au baridi
Maumivu wakati wa tendo la ndoa
Kutokwa na damu isiyo ya kawaida
Mambo ya kufanya ili kuzuia maambukizi
Kupima afya kabla ya kufunga kitanzi – Hakikisha hakuna maambukizi ya uke au mlango wa kizazi kabla ya kuwekewa kitanzi.
Usafi wakati wa kufunga kitanzi – Hakikisha kitanzi kinawekwa na mtaalamu aliye kwenye mazingira safi na salama.
Kutumia kondomu – Kama una wapenzi zaidi ya mmoja au mwenza wako ana wapenzi wengine, tumia kondomu kila mara kulinda dhidi ya magonjwa ya zinaa.
Kufuatilia dalili – Ukiwa na dalili zozote zisizo za kawaida baada ya kufunga kitanzi, wahi kituoni kwa uchunguzi mapema.
Hudhuria kliniki kwa ufuatiliaji – Mara nyingi ufuatiliaji baada ya wiki 4 hadi 6 unashauriwa ili kuhakikisha kitanzi kiko sawa na hakuna maambukizi.
Ikiwa utazingatia ushauri huu, matumizi ya kitanzi ni salama na yenye yenye ufanisi mkubwa katika kuzuia mimba kwa muda mrefu.
Rejea za mada hii
World Health Organization. Selected practice recommendations for contraceptive use. 3rd ed. Geneva: WHO; 2016.
Centers for Disease Control and Prevention (CDC). U.S. Medical Eligibility Criteria for Contraceptive Use, 2016. MMWR Recomm Rep. 2016;65(RR-3):1–103.
Haggerty CL, Ness RB. Epidemiology, pathogenesis and treatment of pelvic inflammatory disease. Expert Rev Anti Infect Ther. 2006;4(2):235–47.
Mohllajee AP, Curtis KM, Peterson HB. Does insertion and use of an intrauterine device increase the risk of pelvic inflammatory disease among women with sexually transmitted infection? A systematic review. Contraception. 2006;73(2):145–53.
Hubacher D, Lara-Ricalde R, Taylor DJ, Guerra-Infante F, Guzmán-Rodríguez R. Use of copper intrauterine devices and the risk of tubal infertility among nulligravid women. N Engl J Med. 2001;345(8):561–7.
Grimes DA. Intrauterine device and upper-genital-tract infection. Lancet. 2000;356(9234):1013–9.