Kiwango cha himoglobin mwilini ni ngapi?
Kiwango cha hemoglobin kwa wanaume ni ngapi
Kiwango cha damu mwilini kwa wanawake ni ngapi?
Kiwango cha damu nyekundu mwilini ni ngapi
Kiwango cha damu kwa mtu mzima ni ngapi?
Kiwango cha damu kwa watoto ni ngapi?
Kiwango cha damu kwa vichanga ni ngapi?
top of page
To test this feature, visit your live site.
Edited: Jul 02, 2021
Kiwango cha damu mwilini ni ngapi?
Kiwango cha damu mwilini ni ngapi?
3 answers0 replies
Like
Maoni (3)
bottom of page
Asante sana.
Kiwango cha damu mwilini
Kiwango cha damu mwilini ambacho hufahamika pia kama 'kiwango che hemoglobin mwilini' hujulikana kwa kuhesabu idadi ya hemoglobin, protini kuu ya chembe nyekundu za damu. Kazi ya hemoglobin ni kubeba oksijeni kutoka kwenye mapafu na kwenda kwenye chembe hai mwilini. Oksijeni ni muhimu sana kwa chembe kwani huziwezesha kutengeneza nishati ya kuendesha shughuli zake kama kuzaliana, kuupa mwili nguvu ya kujongesha misuli n.k. Ili chembe hai ziweze kufanya kazi vema, kiwango cha oksijeni kinapaswa kuwa toshelevu, hii huwezekana endapo kiwango cha hemoglobin kunatosha mahitaji.
Kiwango cha hemoblobin kwa umri
Kiwango cha hemoglobin kwa kawaida hutegemea umri wa mtu, kichanga aliyetimiza 38 hadi 40 za ujauzito anapozaliwa huwa na damu nyingi zaidi kuliko watu wazima au wazee. Jinsi kichanga anavyokuwa, kiwango cha cha hemoglobin hupungua kufikia wastani wa gramu 13 hadi 15 kwa desilita moja ya damu kwa wazee. Kufahamu zaidi kuhusu kiwango cha damu kwa umri, agalia maelezo hapa chini
Umri...............................................................................................Hemoglobin/desilita
(1) Kichanga wa wiki 26 hadi 30 za ujauzito………...............................13.4
(2) Kichanga wa wiki 28………………….....................................................14.5
(3) Kichanga wa wiki 32………………………………......................................15.0
(4) Kichanga aliyetimiza umri wa mimba ( wiki 40)…………………….....17- 22
(6) Kichanga wa siku 1 hadi 3…………………………………………………….....18.5
(7) kichanga wa wiki 2…………………………………………………………………...16.6
(8) Kichanga wa mwezi 1………………………………………………………….......13.9
(9) Kichanga wa miezi 2………………………………………………………………...11.2
(10) Kichanga wa miezi 6……………………………………………………………....12.6
(11) Mtoto wa miezi 6 hadi miaka 2………………………………………….....12.0
(12) Mtoto wa miaka 2 hadi 6…………………………………………………........12.5
(13) Watoto wa miaka 6 hadi 12…………………………………………………....13.5
(14) Watoto/vijana wa kiume miaka 12 hadi 18 ……………………….......14.5
(15) Watoto/vijana wa kikemiaka 12 hadi 18…………………………..….....14.0
(16) Watu mzima(mme) …………………………………………………………………12-18
(17) Mtu mzima (Kike) ……………………………………………………………………12-16
(18) Wazee (Ume) ………………………………………………………………………….12.4 - 15.5
(19) Wazee (kike) ……………………………………………………………………........11.7 - 14.0
Madhaifu ya kiwango cha hemoblobin
Kama ilivyoelezwa hapo juu, ufanyaji kazi wa chembe hai hutegemea oksijeni inayobebwa na hemoglobin, endapo kuna kiwango kidogo cha hemoglobin kwenye damu au kiwango kikubwa zaidi, chembe hai zinashindwa kufanya kazi yake vema na hivyo kuleta dalili mbalimbali za ugonjwa ambazo zimeelezwa kwenye makala zingine ya 'dalili ya upungufu wa damu' na 'damu nyingi mwilini'
Majibu yaliyojibiwa na mada hii
Mada hii imejibu maswali yote yanayohusiana na ;
Kiwango cha himoglobin mwilini
Kiwango cha hemoglobin kwa wanaume
Kiwango cha damu mwilini kwa wanawake
Kiwango cha damu nyekundu mwilini
Kiwango cha damu kwa mtu mzima
Kiwango cha damu kwa watoto
Kiwango cha damu kwa vichanga
Kiwango cha damu kwa vichanga
Rejea za mada hii;
Evaluation of Anemia in Children. https://www.aafp.org/afp/2010/0615/p1462.html. Imechukulia 02.07.2021
Henny H. Billett Chapter 151Hemoglobin and Hematocrit..https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK259/#. Imechukulia 02.07.2021
Lianxiang Ren, et al. Hemoglobin in normal range, the lower the better?—Evidence from a study from Chinese community-dwelling participants. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4014990/. Imechukulia 02.07.2021
Chen Wang, et al. Hemoglobin levels during the first trimester of pregnancy are associated with the risk of gestational diabetes mellitus, pre-eclampsia and preterm birth in Chinese women: a retrospective study. https://bmcpregnancychildbirth.biomedcentral.com/articles/10.1186/s12884-018-1800-7.Imechukulia 02.07.2021