Swali kuu. Nimegundulika kuwa na TB je, ninaweza kujamiiana endapo nimeshaanza dawa?
Maswali mengine yaliyojibiwa kwenye makala hii ni
· Naruhusiwa kushiriki ngona wakati natumia dawa za TB?
· Ni muda gani naruhusiwa kujamiiana baada ya kuanza dawa za TB?
· Ninaweza kufanya ngono endapo natumia dawa za TB?
Jibu:
Hata kama umegundulika kuwa na TB ya kifua iliyogundulika kwa kupima, hatari ya kuambukiza wengine huisha ndani ya wiki 2 hadi 6 tangua kuanza kwa matibabu. Hii ni kweli kwa nadharia kwamba, bakteria waliosababisha TB wanasikia dawa hizo zilizotumika.
Endapo umeshaanza dawa na hali yako ya afya imeimarika, usihofu kuhusu kumwambukiza mwenza kwa kushiriki naye ngono.
Namna kuepuka kuwaambukiza wengine TB
Kwa vile mara baada ya kuanza dawa za TB huchukua wiki chache ili kuingia kwenye kipindi ambacho huwezi kuwaambukiza wengine, unapaswa kufanya mambo yafuatayo ili kuwalinda wengine na kupata maambukizi.
Kaa nyumbani
Usiende kazini, shuleni au kulala chumba kimoja na watu wengine wiki chache baada ya iuanza dawa.
Kaa kwenye chumba chenye hewa ya kutosha
Kwa vile TB husambaa kirahisi mazingira yenye hewa kidogo na mzunguko kidogo wa hewa. Kama chumba unachokaa ni kidogo au mzunguko wa hewa mdogo, fungua madirisha, au tumia feni ili kutoa hewa chafu nje kama hakuna baridi.
Funika kinywaa chako
Tumia tushu au kitambaa kufunika kinywa muda wote unapocheka, kupiga chafya au kukohoa. Tupa kitambaa kilichotumika katika kifuko au chombo chenye mfuniko kisha kitupe.
Vaa barakoa
Barakoa inapaswa kuvaliwa wiki tatu za kwanza baada ya kuanza matibabu ili kupunguza hatari ya kuwaambukiza wengine..
Rejea za mada hii;
1. Basic TB facts. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/tb/topic/basics/default.htm. Imechukuliwa 22.05.2022
2. Barua M, Van Driel F, Jansen W. Tuberculosis and the sexual and reproductive lives of women in Bangladesh. PLoS One. 2018;13(7):e0201134. Published 2018 Jul 19. doi:10.1371/journal.pone.0201134
3. Jameson JL, et al., eds. Tuberculosis. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 20th ed. McGraw-Hill; 2018. http://accessmedicine.com. Imechukuliwa 22.05.2022
4. Tintinalli JE, et al., eds. Tuberculosis. In: Tintinalli's Emergency Medicine: A Comprehensive Study Guide. 9th ed. McGraw Hill; 2020. http://www.accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 22.05.202
5. Tuberculosis (TB): Questions and answers about TB. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/tb/publications/faqs/qa_tbdisease.htm. Imechukuliwa 22.05.2022
Ninaruhusiwa