Je ni wiki ngapi zinatakiwa kupita ili nijifungue?
Inachukua wiki ngapi za ujauzito ili kujifungua mtoto kamili?
Kujifungua ni siku ngapi za ujauzito?
Wiki ya kujifungua
Wiki ya kujifungua mtoto wa kiume
Wiki ya kuzaa mtoto
Video inayofuata ina maelezo kuhusu kujifungua ni wiki ngapi.
Wiki za ujauzito
Ili kuweza kujibu swali vema, ni vema nikauliza swali na kulijibu ili kupata msingi mzuri
Je Binadamu anabeba mimba kwa siku au wiki ngapi za ujauzito?
Inakadiliwa kuwa binadamu hubeba mimba kwa muda wa wiki 40 sawa na siku 280 na ni sawa pia na miezi 10 kamili kama utahesabu mwezi kuwa na siku 28 ( au miezi 9 siku 6 na masaa 6 kwa mwezi wenye siku 30 au 31).Makadilio haya si lazima kila mtu ayafikie, kuna baadhi ya wanawake wanaweza kujifungua kabla ya kipindi cha siku hizi 40.
Tarehe ya matazamio ya kujifungua huhesabishwa kwa kukadilina wiki hizi 40, hii ndio maana wanawake wengi wanaweza wakajifungua kabla au baada ya hizo tarehe.
Ni wakati gani sahihi wa kujifungua?
Mtoto husemekana kuwa amekomaa na anaweza kuishi akifikisha muda wa wiki 35 na kuendelea, katika kipindi cha wiki hizi, mapafu huwa yamekomaa na mtoto anaweza kupumua mwenyewe bila kuhitaji mashine.
Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa, mama anatakiwa kufikisha angalau wiki 39 hadi 41 kwa sababu tu watoto wanaozaliwa katika wiki hizi hupata maudhi machache ukilinganisha watoto waliojifungu kabla au baada ya wiki hizo.
Wakati sahihi wakujifungua ni pale utakapopata uchungu asilia baada ya wiki 37 za ujauzito ambapo mtoto anakuwa amekomaa mapafu na viungo vingine na hivyo anaweza kuishi.
Ni wakati gani itasemekana umewahi kujifungua?
Endapo utajifungua chini ya wiki 37 za ujauzito, utasemekana kuwa umejifungua kabla ya wakati na utapata mtoto njiti. Baadhi ya nchi zenye uwezo wa kutunza watoto njiti, mama anaweza kujifungua kuanzia wiki ya 23 hadi 28 na akaishi chini ya uangalizi maalumu na kwa kutumia vifaa maalumu vya kumpa mtoto joto na chakula. Hata hivyo kwenye nchi nyingi zinazoendelea ambazo hazina vifaa vya kutunza watoto njiti, endapo mama amepata uchungu kwenye wiki chini ya 28 au akiwa chini ya kilo moja, mtoto huyu ni nadra sana kuishi.
Ni wakati gani itasemekana umechelewa kujifungua?
Endapo utajifungua baada ya wiki 40 za ujauzito, utasemekeana kuwa umechelewa kujifungua hivyo utahitaji kuanzishiwa uchungu. Baadhi ya wataalamu huacha mpaka itakapofikia wiki ya 41 au 42 ndipo kuanzisha uchungu endapo haujaanza wenyewe au kujifungua kwa upasuaji.
Rejea za mada hii
March of Dimes. Why at least 39 weeks is best for your baby - https://www.marchofdimes.org/pregnancy/why-at-least-39-weeks-is-best-for-your baby.aspx#:~:text=Depending%20on%20your%20health%20and,to%20begin%20on%20its%20own. Imechukuliwa 19.06.2021
How Early Can You Safely Give Birth?. https://www.healthline.com/health/pregnancy/how-many-weeks-is-it-safe-to-give-birth. Imechukuliwa 19.06.2021
Definition of term pregnancy. acog.org/Clinical-Guidance-and-Publications/Committee-Opinions/Committee-on-Obstetric-Practice/Definition-of-Term-Pregnancy?IsMobileSet=false. Imechukuliwa 19.06.2021
Deliveries before 39 weeks. acog.org/About-ACOG/ACOG-Departments/Deliveries-Before-39-Weeks?IsMobileSet=false. Imechukuliwa 19.06.2021
Extremely preterm birth. acog.org/Patients/FAQs/Extremely-Preterm-Birth?IsMobileSet=false. Imechukuliwa 19.06.2021
Mwanamke aliyepata period kwa wiki 3 je alafu akabeba mimba anaweza akajifungua hyo tarehe ya makadirio au anaweza akapitiliza