Nina tatizo la kukojoa damu badala ya shahawa kwenye tendo la ndoa na sina maumivu yoyote wala ugonjwa wa zina wowote je shida ni nini?
HIli ni swali ambalo limeulizwa mara kwa mara na watumiaji wa tovuti ya ULY CLINIC. Majibu yake ningependa kuyaelezea hapa chini
Mwanaume anapo mwaga mbengu wakati wa kujamiana, mbengu hizo huwa na mchanganyiko wa majimaji yaliyotolewa katika tezi mbalimbali kwenye mfumo wa uzalishaji mbegu ikiwapo tezi dume. Shahawa na majimaji hupita katika mirija mbalimbali hadi kufikia kwenye mrija unatoa mkojo nje ya mwili yaani urethra, njia hizi huwa na mishipa ya damu na hivyo endapo kuna tatizo katika mirija hiyo kama maambukizi au matatizo mengine mbalimbali, hupelekea kuvilia damu ndani ya mirija na kuonekana kama mchanganyiko wa damu kwenye shahawa au mkojo.
Soma zaidi kuhusu visababishi kwa kubonyeza hapa