Ukweli kuhusu wiaini nyekundi na kukukinga na magonjwa ya moyo
Kunywa waini nyekundu kwa kiasi imekuwa ikifikiriwa kuwa na umuhimu kwa afya ya moyo.
Pombe na aina fulani ya kemikali zilizo kwenye waini nyekundu zinazoitwa antioxidanti huweza kusaidia kukukinga dhidi ya magonjwa ya mishipa ya moyo ya koronari ambayo huweza kupelekea mshituko wa moyo.
Uhusiano kati ya waini nyekundu na kupunguza mshituko wa moyo bado haujajulikana vema. Hata hivyo faida mojawapo inajulikana kuwa antioksidant zilizo kwenye wine nyekundu huweza kuongeza kiwango cha kolestro aina ya HDL ambayo hufanya kazi ya kuosha damu kwa kuondoa kiwango cha kolestro aina ya LDL ambayo ikiwa kwa kwiango kikubwa mwilini hupelekea kujishikiza kwa Mafuta kwenye mishipa ya damu ya moyo(koronari) hata kuziba kwa mishipa hiyo. Mishipa ya damu inapoziba au endapo Mafuta yakachomoka kwenye ukuta wa mishipa ya damu, huweza kuziba mishipa ya damu midogo kwenye moyo hivyo kuleta mshituko wa moyo au kiharusi endapo mishipa midogo ya ubongo imeziba.
Hata hivyo, waini nyekundu huwa na kemikali inayoitwa polyphenol aina ya resveratrol ambayo hulinda kuta za ndani za mishipa ya damu. Kama ilivyoelezewa hapo juukwa kupunguza kiwango cha LDL.
Kemikali ya resveratrol hupatikana kwenye kwenye badhi ya mimea na matunda. Huzalisha na mimea wakati wa hatari, kama vile wakati mmea umevamiwa na vimelea vya bakteria au fangasi ili kupambana na adui hawa. Vyakula na matunda yenye kemikali hii ni kama vile zabibu, matunda ya madogo kama forosadi na yanayofanana na forosadi, blueberries, mulberries na karanga.
Ni kiwango gani cha pombe unatakiwa kunywa?
Kiwango cha pombe unachotakiwa kunywa kitaalamu inategemea jinsia yako. Soma Zaidi mada hii kwenye mada ya pombe na afya ya mwili wako kwenye tovuti hii.