Swali:
Je, kukitumia maji mengi hupunguza gono?
Je, kunywa maji mengi hutibu gono?
Jibu:
Gono ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na maambukizi ya bakteria mwenye jina la neisserian gonorrhoea. Maambukizi hutokea pale mtu anaposhiriki ngono na mtu mwenye maambukizi pasipo kutumia kinga.
Kwa wanaume, Bakteria anayesababisha gono anapoingia kwenye njia ya mkojo huanza hujizalia na kushambulia mrija huo kwa kuingia ndani na kuta zake.
Matibabu ya gono
Matibabu pekee ya gono ni kutumia dawa zenye nguvu ya kuua bakteria hao na katika dozi na maelekezo maalumu ya daktari.
Jibu la msingi
Kwa kuwa kunywa maji mengi huambatana na kupata mkojo mwingi unaotoka kupitia mrija wa mkojo wa mwanaume, baadhi ya vimelea wa gono ambao hawajajishikiza kwenye kuta ya mrija wa mkojo hutolewa kwenye njia hiyo wakati wa kukojoa.
Hitimisho
Kutokana na maelezo hapo juu, kunywa mani mengi hakuondoi wala kutibu gono.
Soma maelezo zaidi kuhusu gono na matibabu yake sehemu nyingine ya tovuti hii.