Vipimo vya kupima UKIMWI jamii ya SD bioline hupima uwepo wa antibodi zinazozalishwa na mwili ili kushambulia virusi vya UKIMWI.
Namna ya kupima UKIMWI kwa kutumia mate
Chukua kichukua sampuli ya mate kisha pitisha kwenye fizi za juu na chini mara moja ili kukusanya sampuli kisha
Weka sampuli yako kwenye kipimo, sehemu ya kuweka sampuli
Endapo sampuli ni ya kutosha, haina haja ya kuweka bafa ( endapo sampuli ni kidogo weka matone 2 ya bafa
Subiri sampuli itembee kwenye kipimo
Soma majibu ya kipimo ndani ya dakika 20
Tafiti zinaonyesha, matumizi ya mate inaweza kuwa njia mbadala na isiyo ya kuumiza dhidi ya njia ya kutumia damu. Kupima UKIMWI kwa kutumia mate huweza kutambua uwepo wa virusi vya UKIMWI kwa asilimia 99.
Endapo una kipimo maalumu cha kutumia mate, pitisha kichukua sampuli mara moja kweney fizi za juu, kisha fizi za chini na kisha kiunganishe kwenye kipimo chako na soma majibu ndani ya dakika 20.
Kumbuka:
Kupima UKIMWI Kwa kutumia mate inahitaji uwe na kipimo ambacho kimetengenezwa madhubuti kwa ajili ya kupima uwepo antibodi za VVU kwenye mate, endapo utatumia kipimo kisicho sahihi unatoa uwezekano wa kupata majibu yasiyo sahihi.
Vp
Jinsi ya kupima UKIMWI kwa kutumia mate;

Rejea za mada hii
Willfried Schramm, et al. A Simple Saliva-Based Test for Detecting Antibodies to Human Immunodeficiency Virus. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC95731/. Imechukuliwa 14.06.2021
Puneeta Vohra, et al. Evaluation and diagnostic usefulness of saliva for detection of HIV antibodies: A cross-sectional study. https://www.jfmpc.com/article.asp?issn=2249-4863;year=2020;volume=9;issue=5;spage=2437;epage=2441;aulast=Vohra. Imechukuliwa 14.06.2021
How accurate is the rapid oral HIV test?. https://www.hiv.va.gov/patient/faqs/rapid-oral-test-accuracy.asp. Imechukuliwa 14.06.2021
Saliva May Be a Reliable Alternative to Blood for HIV Antibody. https://www.ajmc.com/view/saliva-may-be-a-reliable-alternative-to-blood-for-hiv-antibody-testing#. Imechukuliwa 14.06.2021
Scientists Zero in on Better Saliva-Based HIV Test. https://www.webmd.com/hiv-aids/news/20180129/scientists-zero-in-on-better-saliva-based-hiv-test. Imechukuliwa 14.06.2021
How Oral HIV Testing Works | OraQuick In Home HIV Test. http://www.oraquick.com/what-is-oraquick/how-oral-testing-works. Imechukuliwa 14.06.2021