Kutapika matapishi ya rangi nyeusi huitwa kutapika nyongo nyeusi na baadhi ya watu. Kutapika nyongo nyeusi au kutapika matapishi ya rangi nyeusi ni hali inayomaanisha kutapika damu iliyokwisha meshameng’enywa na tindikali tumboni. Matapishi pia yanaweza kubadilika na kuwa na rangi inayofanana na unga wa kahawa.
Damu iliyovilia tumboni kisha kukutana na tindikali humeng’enywa na hivyo hupata rangi nyeusi. Endapo mtu atatapika matapishi yenye rangi nyeusi bila wekundu, hii inamaanisha kuwa damu inavia kidogo sana au imekatika muda mrefu kabla ya kutapika.
Visababishi vya kutapika nyongo nyeusi
Visababishi vya kutapika nyongo nyeusi ni vile ambavyo vinasababisha damu kuvia ndani ya tumbo ambavyo baadhi yake vinavyotokea sana na kufahamika ni;
Maambukizi ya fangasi kwa wanaotumia dawa za kushusha kinga za mwili kama wagonjwa wa saratani
Visababishi vya kutapika nyongo nyeusi kwa watoto ni;
Kutostahimili chakula
Damu kutoka kwenye majeraha ndani ya kinywa
Madhaifu ya kuganda kwa damu
Madhaifu ya kuzaliwa kwenye mfumo wa mumeng’enyaji chakula au mishipa ya damu
Visababishi vya kutapika nyongo nyeusi kwa watu wazima
Majeraha kwenye kinywa, koo, fizi kutokana na kukohoa n.k
Vidonda vya tumbo au vidonda katika sehemu yoyote ya mfumo wa umeng’enyaji wa chakula
Ugonjwa wa amilaidosis
Kuferi kwa Ini ambako huonekana na dalili zingine kama manjano n.k
Majeraha ya umio kutokana kutapika kwa nguvu au sana
Wakati gani wa kuonana nadaktari unapokuwa unatapika matapishi ya rangi nyeusi?
Wasiliana na daktari wako haraka endapo unatapika matapishi ya rangi nyeusi pamoja na dalili za;
Kizunguzungu
Kupumua kwa shinda
Unatapika nyongo kwa muda mrefu
Unatapika zaidi ya masaa 48 bila kupata nafuu
Unatapika kila kitu
Maumivu makali ya tumbo nay a ghafla
Una kisukari
Unapata maumivu makali ya kifua
Unavipindi vya kutapika mara kwa mara katika mwaka
Damu nyekundu kwenye matapishi
Maumivu makali ya kichwa na homa
Kuishiwa nguvu au kupata uchovu mkali
Kupata kizunguzungu au kuzimia
Huduma ya kwanza kwa mtu anayetapika
Hatua ya muhimu kuchukua endapo unatapika sana ni kufika hospitali ili kupatiwa matibabu kw akutundikiwa dripu, hii itasaidia rejesha kiwango cha madini na maji ulichopoteza.
Kama unatapika kwa kiasi na unaweza kunywa maji, fanya iwezekanavyo kunywa maji kiasi kidogo sana lakini mara kwa mara. Ukipata maji ya Oral au wengine huita ORS na hutumika kwa watoto wanaoharisha itasaidia kuwa kama huduma ya kwanza. Kengo ni kurejesha kiwango ulichopoteza kwa kutapika na kuzuia kupata shoku kutokana na kuishiwa maji mwilini.
Epuka vitu vinavyokuletea kichefuchefu kama vinywaji nyenye mafuta, sukari na viungo kwa wingi na vingine.
Rejea za mada hii;
Vomiting in adults. https://www.nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021
Catiele Antunes, et al. Upper Gastrointestinal Bleeding. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK470300/#. Imechukuliwa 28.06.2021
I.Dodd Wilson. Chapter 85Hematemesis, Melena, and Hematochezia. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK411/. Imechukuliwa 28.06.2021
Amyloidosis. my.clevelandclinic.org/health/diseases/15718-amyloidosis. Imechukuliwa 28.06.2021
Cyclic vomiting syndrome. niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/cyclic-vomiting-syndrome. Imechukuliwa 28.06.2021
Lamps LW, et al.Fungal infections of the gastrointestinal tract in the immunocompromised host: An update. DOI: 10.1097/PAP.0000000000000016. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff. Acute liver failure. mayoclinic.org/diseases-conditions/acute-liver-failure/symptoms-causes/syc-20352863. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff. Viral gastroenteritis (stomach flu). https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/viral-gastroenteritis/symptoms-causes/syc-20378847. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Food poisoning. mayoclinic.org/diseases-conditions/food-poisoning/symptoms-causes/syc-20356230. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Gastritis.mayoclinic.org/diseases-conditions/gastritis/symptoms-causes/syc-20355807. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Gastroesophageal reflux disease (GERD). mayoclinic.org/diseases-conditions/gerd/symptoms-causes/syc-20361940. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Intestinal obstruction. mayoclinic.org/diseases-conditions/intestinal-obstruction/symptoms-causes/syc-20351460. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Nausea and vomiting. mayoclinic.org/symptoms/nausea/basics/definition/sym-20050736. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Vomiting blood. mayoclinic.org/symptoms/vomiting-blood/basics/definition/sym-20050732
Nausea and vomiting in adults. nhs.uk/conditions/nausea-and-vomiting-in-adults/. Imechukuliwa 28.06.2021
Nausea and vomiting. my.clevelandclinic.org/health/symptoms/8106-nausea--vomiting. Imechukuliwa 28.06.2021
Vomit looks like coffee grounds after drinking alcohol. goaskalice.columbia.edu/answered-questions/vomit-looks-coffee-grounds-after-drinking-alcohol. Imechukuliwa 28.06.2021
Vomiting in adults. (2018). nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021