Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wengi hutokwa damu kwa wastani wa siku 14 tangu kutumia dawa ya kutoa mimba. Hata hivyo idadi ya siku ambazo matone madogo ya damu hutoka huweza kwenda hadi siku 10 zaidi.
Kiasi cha damu kinachotoka baada ya kutoa mimba kwa kutumia dawa kinaweza kufanana na kiwango cha damu ya hedhi ya kawaida au hedhi nzito ikitegemea na umri wa mimba na sababu zingine.
Mabonge ya damu
Katika Makala hii, neno damu nyingi, damu kidogo na mabonge ya damu yametumika kuelezea wingi wa damu kwa kufananisha na matunda:
Bonge dogo ukubwa wa zabibu ni sawa na damu kidogo
Bonge dogo ukubwa wa ndimu ni sawa na damu kiasi
Bonge la ukubwa wa chungwa ni sawa na damu nyingi sana
Ni wakati gani damu huanza kutoka?
Mara baada ya kumeza dawa na kuweka kwenye shingo ya kizazi, wanawake wengi hutokwa na damu kati ya nusu saa hadi masaa 10. Wastani wa masaa ya kutokwa damu ikiwa ni masaa 2 hadi 4.
Kipindi cha kutoka damu nyingi kinaweza kudumu kwa muda wa saa 1 hadi 4 wakati mimba inatolewa nje ya kizazi. Baadhi ya wanawake damu nyingi zinaweza kuendelea kutoka kwa siku chache hadi wiki kadhaa.
Wanawache wachache pia wanaweza kupata kipindi cha pili cha kutokwa damu wiki kadhaa baada ya kumeza dawa.
Sifa na muda wa kutoka damu
Damu huwa nyepesi au kutotoka kabisa kwa siku 3 za kwanza baada ya kutuma dawa
Damu inaweza kuwa nzito siku ya 4 au 5 na kuambatana na mabonge meusi, na maumivu ya tumbo
Damu kidogo au matone yanaweza kuendelea kutoka kwa muda wa wiki 2 hadi 4
Damu huweza kuongezeka kwa kufanya kazi ya kuushughulisha mwili
Sifa za mabonge ya damu
Huweza kuwa ukubwa wa ndimu na kutoka muda wowote ndani ya wiki 4 toka kutumia dawa
Sifa za maumivu ya tumbo
Hupotea kwa kukanda na maji ya moto au kutumia dawa za maumivu.
Ni wakati gani uonane na daktari haraka?
Wasiliana na daktari wako haraka endapo dalili au ishara zifuatazo zinatokea.
Kulowanisha taulo ya kike nne au Zaidi ndani ya masaa 2
Kutokwa na mabonge makubwa ya damu( karibia ukubwa wa ndimu ndogo)
Kupata homa au joto la mwili kupanda zaidi ya digrii za selishias 38.0
Kutetemeka mwili ndani ya masaa 24 toka kutumia dawa
Kutokwa na ute usio wa kawaida ukeni kama vile ute wa kijani au njano
Makala hii imejibu maswali yafuatayo
Je inachukua muda gani damu kukatika baada ya kutoa mimba kwa dawa?
Je ni kiasi gani cha damu hutoka baada ya kutoa mimba kwa dawa?
Je , damu inakatika lini baada ya kutoa mimba kwa dawa?
Je, damu inaanza kutoka lini baada ya kutumia dawa za kutoa mimba?
Je ni dalili gani ya hatari baada ya kutoa mimba kwa dawa?
Je kutokwa na mabonge ya damu ni kawaida baada ya kutoa mimba kwa dawa?
Mambo mengine unayopaswa kufahamu baada ya kutoa mimba
Baada ya kutoa mimba unaweza kupata mimba nyingine mara moja, hivyo utapaswa kutumia kinga ili kuzuia mimba nyingine. Linki ifuatayo ina video zinazoainisha siku za hatari kulingana na mzunguko wako wa hedhi. Bofya kiungo cha makala husika hapa chini ili kufahamu ni lini unaweza kushika ujauzito hivyo uchukue hatadhari.
Rejea za mada
Davis A, Westhoff C, De Nonno L. Bleeding patterns after early abortion with mifepristone and misoprostol or manual vacuum aspiration. J Am Med Womens Assoc (1972). 2000;55(3 Suppl):141-4. PMID: 10846324.
https://womenshealthclinic.org/what-we-do/abortion/after-an-abortion/. Imechukuliwa 25.01.2023
National Abortion Federation (2008) Early Medical Abortion; in Clinical Policy Guidelines Washington, DC; pp 7-11.
Breitbart V, Repass DC. The counseling component of medical abortion. J Am Med Womens Assoc
2000; 55(suppl 3):164-166.
Creinin MD. Randomized comparison of efficacy, acceptability and cost of medical versus surgical abortion. Contraception 2000; 62:117-24.
Henderson JT, Hwang AC, Harper CC et.al. (2005) Safety of mifepristone abortion in clinical use. Contraception 72:175-8.
Chen AY, Mottl-Santiago J, Vragovic O et.al. (2006) Bleeding after medication-induced termination of pregnancy with two dosing schedules of mifepristone and misoprostol. Contraception 73: 415-19.
Allen RH, Westhoff C, DeNonno L, Fielding SL, Schaff EA. Curettage after mifepristone-induced abortion: Frequency, timing, and indications. Obstet Gyncecol 2001;98:101-6.
Schaff EA, Fielding SL, Westhoff C, Ellertson C, Eisinger SH, Stadalius LS, Fuller L. Vaginal misoprostol administered 1, 2, or 3 days after mifepristone for early abortion. JAMA 2000;284:1948-1953.
Habari wapendwa mimi ninetumia misoprostal ile yenye vidonge vitano nilipewa maelekezo kimoja nameba after 24hrs nameza zile nne zote kwa wakati mmoja ila tangu Jana mpka sasa sijaona dam wala chochote ila najisikia vibaya mwili hauna nguvu na maumivu ya tumbo 🙏😓msaada please
Baada ya kutumia dawa ya kutoa mimba damu imetoka kidogo sana je ni sawa