Swali: Nilifanya mapenzi na mdada, asubuh yake baada ya kwenda kuoga wakat nakojoa nilipata kuona cream ndogo sana kabla sijakojoa inakuana rangi kama ya shahawa hii ni dalili ya nini? Ila maumivu hamna.
Visababishi vya kutoka na ute mweupe
Kutokana na maelezo katika makala hii, visababishi vya kutokwa na ute mweupe vinaweza kuwa vile vya kawaida au visivyo vya kawaida.
Visababishi vya kawaida
Kuna uwezekano mkubwa kwamba ute uliotoka kwenye uume asubuhi wakati anaoga unatokana na mabaki ya manii ambayo hayakutoka yote wakati amemaliza kujamiana.
Visabaishi visivyo kawaida
Visababishi visivyo vya kawaida vya kutokwa na ute katika makala hii inaweza kuwa maambukizi kwenye mfumo wa mkojo haswa maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama;
Hata hivyo dalili zingine na vihatarishi vinaweza kuwepo kudhihirisha kuwa kutokwa na ute kunatokana na maambukizi hayo. Bofya ugonjwa husika kwa maelezo ya vihatarishi na dalili zingine zinazoweza ambatana na magonjwa hayo.
Ili kupata maelezo zaidi pia, unapaswa kuwasiliana na daktari wao siku zote kabla ya kuchukua hatua.
Pia unaweza wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia namba za simu zilizo chini ya tovuti hii au kwa kubofya linki ya Pata tiba chini ya tovuti hii.