Ni kawaida mwanamke kutokwa na ute mweupe usio na harufu au wenye harufu kiasi kabla na wakati wa ujauzito. Hali ya kutokwa na ute huongezeka wakati wa ujauzito kutokana na ongezeko la homoni estrojeni kwenye damu inayotoa maelekezo ya kuongeza uzalishaji wa ute huu ukeni.
Aidha kutokwa na ute ukeni si tu kunaweza maanisha uwepo wa mimba, bali unaweza maanisha mwanamke anaingia kwenye kipindi cha uovuleshaji endapo hana mimba. Kipindi cha uovuleshaji ni kipindi cha hatari kushika mimba kinachodumu kwa masaa 24 hadi 36. Mwanamke akishiriki ngono wakati huu anaweza kubeba ujauzito.
Â
Sifa za ute mweupe ulio kawaida wakati wa ujauzito
Mara nyingi huwa mweupe kama maji au karatasi
Hauna harufu au kuwa na harufu kiasi
Awali huwa mzito na baadae huwa mwembamba
Huongezeka ujauzito unavyokuwa
Â
Ute mweupe wakati wa uovuleshaji
Huwa na sifa zifuatazo
Mweupe
Huwa mzito awali na baadae huwa mwembamba na kuteleza
Huweza kuonekana na weupe wa ute wa yai
Huwa hauna harufu
Huwa hauleti bugudha
Â
Dalili nyingine za mimba
Dalili zingine za ujauzito ni pamoja na;
Kutokwa damu
Mabadiliko ya chuchu kama kuvimba, na kuuma
Kichefuchefu na kutapika
Kutoingia mwezini
Kutokwa matone ya damu
Mumivu ya tumbo la chini
Hisia za uchovu
Â
Je, unathibitishaje kuwa una mimba?
Ili kuthibitisha kuwa una ujauzito, unapaswa kufanya vipimo. Kwa wiki za awali, vipimo vya sasa vya mkojo huwa havionyeshi uwepo wa mimba, hivyo utabidi kufanya ultrasound. ENdapo kipimo cha ultrasound kitafanyika na mtaalamu, ataweza kuona dalili za uwezo wa mimba.
Rejea za mada hii
How much vaginal discharge is normal? (2024). https://www.plannedparenthood.org/blog/how-much-vaginal-discharge-is-normal. Imechukuliwa 17.11.2024
ULY CLINIC. Dalili za ujauzito. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ujauzito . Imechukuliwa 17.11.2024
ULY CLINIC. Dalili za ujauzito wa wiki moja. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/dalili-za-ujauzito-wa-wiki-moja. Imechukuliwa 17.11.2024
Signs and symptoms of pregnancy. (2022).
https://www.nhs.uk/pregnancy/trying-for-a-baby/signs-and-symptoms-of-pregnancy/. Imechukuliwa 17.11.2024
Vaginal discharge. (2024). https://www.nhs.uk/conditions/vaginal-discharge/. Imechukuliwa 17.11.2024
Vaginal discharge during pregnancy. (2022). https://www.pregnancybirthbaby.org.au/vaginal-discharge-during-pregnancy. Imechukuliwa 17.11.2024