Miwasho sehemu za siri ni nini kisababishi?
Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha muwasho ukeni. Watu wengi wamekuwa wakifahamu muwasho ukeni husababishwa na maambukizi ya fangasi tu, hii sio sahihi kwa kuwa kuna visababishi vingine vingi vinavyochangia. Tatizo la muwasho ukeni ni kubwa na hupelekea mwanamke kupatamatatizo ya kisaikolojia kwa kuwa mara nyingi inakuwa vigumu wakati mwingine kusema kwa daktari kwamba nina tatizo sehemu zangu za siri. Hata hivyo endapo una tatizo la kuwashwa ukeni, hupo peke yako na daktari anaweza kukusaidia kupata tiba rahisi itakayoondoa tatizo lako na kukupa uhuru zaidi na kujiamin.
Visababishi vya kuwashwa uke
Muwasho ukeni ni ishara ya mwitikio wa mwili kwenye maambukizi au kitu kigeni sehemu za siri. Visabaishi vinaweza kuwa;
Huleta dalili ya muwasho pamoja na hisia za kungua , kutoa harufu mbaya kama samaki aliyeoza na kutoa uchafu ukeni wa rangi tofauti
Magonjwa ya zinaa
Hutokea sana kwa wanawake wanaotumia sana dawa za antibayotiki au kuwa na kinga za mwili za chini
Mzio(allergy) na uchafu au manukato mbalimbali
Pedi za kutia ukeni ( tampoon)
Manukatoya kutia ndani ya uke
Nguo jamii ya nylon na polyester
Magonjwa ya ngozi kwenye mashavu ya uke
Lichen Sklerosaz
Lichen planaz
Soriasis
Muwasho wa ujauzito
Pemphigoid Gestationis
Ezima
Michomo ya kusinyaa kwa mashavu ya uke
Maambukizi ya streptococcus
Unawezaje kutambua kisababishi halisi cha muwasho uke?
Ili uweze kutambua kisababishi cha muwasho ukeni, unatakiwa kufahamu kuhusu sifa za magonjwa yaliyoandikwa haswa dalili zake na mwonekano wake na wakati mwingine unahitaji kuthibitisha kwa vipimo. Daktari wako anaweza kutambua kwa kuchukua historia yako na kufanya uchuguzi wa awali ukeni au kuagiza vipimo kufanyika.
Ufanye nini endapo una muwasho ukeni?
Endapo una muwasho ukeni, wasiliana na daktari wako kwa uchunguzi na tiba kabla ya kutumia dawa yoyote
Matibabu ya muwasho ukeni
Kwa sababu kuna visababishi vingi vya miwasho ukeni, baada ya daktari wako kuchukua historia ya tatizo lako na kukufanyia vipimo atakupa tiba kutokana na kisababishi. Dawa utakazopewa zinaweza kuwa za kupunguza dalili ya muwasho na dawa za kutibu maambukizi ukeni au dawa za kutibu maambukizi tu.
Dawa za kuficha muwasho ukeni
Dawa zifuatazo huficha muwasho ukeni lakini kamwe hazitibu kisababishi;
Krimu ya Hydrocortisone
Diphenhydramine
Benzocaine
Ciclosporin
Triamcinolone
Doxepin
Fluoxetine
Sertraline
Dawa za kutibu maambukizi
Endapo maambukizi ya fangasi ndo kisababishi, dawa za antifango zitatumika, zinaweza kuwa kati ya;
Terbinafine
Butenafine
Dawa ya kupaka ya Clotrimazole
Miconazole
Ketoconazole
Dawa ya kupaka ya Econazole
Luliconazole
Naftifine
Oxiconazole
Tolnaftate
Ciclopirox
Itraconazole
Sulconazole
Griseofulvin
Dawa hizi zinaweza kuwa za kupaka, kunywa au kidonge cha kuweka ukeni, utashauriwa na daktari ni dawa gani itakufaa kulingana na umri wako, hali ya ujauzito na ukubwa wa tatizo
Maambukizi ya vajinosisi ya bakteri
Hutibiwa kwa dawa za antibayotiki kama;
Metronidazole
Tinidazole
Maambukizi ya magonjwa ya zinaa ya bakteria
Magonjwa ya zinaa kama kisonono, kaswende na trikomoniasis yanayosababishwa na bakteri hutibiwa kwa dawa za antibayotiki kama vile;
Penicillin G
Azithromycin
Doxycycline
Ceftriaxone
Metronidazole
Tinidazole
Azithromycin
Cefixime
Cefotaxime
Ceftizome
Erythromycin
Gemifloxacin
Gentamicin
Soma zaidi kuhusu magonjwa ya zinaa na matibabu yake kwa kubofya hapa
Magonjwa ya zinaa ya virusi
Magonjwa ya zinaa kutokana na virusi hayana tiba ponyaji mpaka sasa, hata hivyo kuna dawa za kupunguza dalili za ugonjwa kwa kuzuia kuzaliana sana kwa virusi ambazo ni;
Inosine pranobex
Acyclovir
Famciclovir
Valaciclovir
Gancyclovir
Dawa asilia za muwasho ukeni
Kuna dawa za asili za muwasho ukeni unaweza kuandaa mwenyewe au kununua kutoka kwenye maduka mbalimbali ya dawa asilia, baadhi ya dawa hizo ni;
Namna ya kuthibiti na kujikinga na muwasho ukeni
Baadhi ya watu huwa na muwasho ukeni kwa sababu ya uchafu au matumizi ya vichokoza ngozi ukeni, vichokoza ngozi husababisha mzio wa ngozi ya uke. Huweza kuwa sabuni kali n.k endapo unawashwa uke, unaweza kutumia mbinu zifuatazo kama matibabu ya nyumbani ya kuwashwa uke;
Tumia maji ya kawaida kujiosha uke badala ya sababuni au vitakasa kusafishia uke. Uke una njia asili ya kujisafisha, na hauhitaji kutakaswa kwa sababuni au kemikali zozote
Tumia pedi za kawaida ambazo si za kuchomeka ndani ya uke
Vaa nguo za ndani zisizobana na haswa zilizotengenezwa na pamba. Nguo za nylon huleta joto ukeni na pia nyuzi zake huchokoza ngozi na kusababisha muwasho
Hakikisha unabadilisha nguo za ndani kwa wakati, usirudie nguo ile ile kila siku
Usiweke manukato ndani ya uke
Baada ya kushuriki ngono bila kinga, hakikisha unajisafisha kwa maji safi tu, isipokuwa endapo unataka kupata mimba
Tumia dawa za kupaka kama, Krimu ya Calcipotriene, Pimecrolimus au tacrolimus kwa magonjwa ya ngozi yanayosabaishwa na soriasis
Kudhibiti muwasho ukeni kutokana na magonjwa ya ngozi
Ili kudhibiti kuwashwa ukeni kutokana na magonjwa ya ngozi kabla ya kuonana na daktari wako unaweza kutumia njia zifuatazo;
Paka dawa za kununua duka la dawa muhimu jamii ya corticosteroid au antihistamine ili kuficha muwasho
Paka mafuta jamii ya petroleum(kama mafuta ya vasselin blue seal yasiyotiwa pafumu) au aquaphor
Safisha taratibu eneo lenye muwasho kilasiku na kausha, usitumie sabuni au manukato makali au kusafisha mara kwa mara
Ondoa hisia za kuungua kwa kutumia mafuta au kukalia maji ya uvuguvugu, barafu au kitambaa cha maji baridi
Zuia mkojo kugusa mashavu ya uke, baadhi ya magonjwa ya ngozi yanapoguswa na mkojo maumivu au muwasho huzidi zaidi mfano soriasis
Majina mengine yanayotumika kumaanisha tatizo la kuwashwa ukeni
Baadhi ya watu hutumia majina haya kumaanisha kuwashwa ukeni
Muwasho ukeni
Kujikuna ukeni
Kuungua ukeni
Kuungua uke
Kuwashwa uke
Kuwashwa mashavu ya uke
Kuwashwa ndani ya uke
Kujikuna mashavu ya uke
Dawa za muwasho ukeni
Dawa ya uke unaowasha
Rejea za mada hii
Linn Woelber, et al. Vulvar Pruritus—Causes, Diagnosis and Therapeutic Approach. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7081372/. Imechukuliwa 02.07.2021
Julien Lambert. Pruritus in Female Patients. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3966341/. Imechukuliwa 02.07.2021
ULY CLINIC. Maambukizi ya fangasi ukeni. https://www.ulyclinic.com/fungasi-ukeni. imechukuliwa 02.07.2021
ULY CLINIC.Magonjwa ya zinaa. https://www.ulyclinic.com/magonjwa-na-saratani/Magonjwa-ya-zinaa. imechukuliwa 02.07.2021
ULY CLINIC. Miwasho sehemu za siri-ukeni. https://www.ulyclinic.com/miwsho-ukeni. Imechukuliwa 02.07.2021
Dawa za utibu gono. https://www.ulyclinic.com/dawa-gono. Imechukuliwa 02.07.2021
ULY CLINIC. Dawa za kutibu herpes. https://www.ulyclinic.com/dawa-za-herpes-na-varicella-zoster. Imechukuliwa 02.07.2021
ULY CLINIC. Dawa za kutibu fangasi maeneo ya siri. https://www.ulyclinic.com/dawa-za-kutibu-fungus-maeneo-ya-sir. Imechukuliwa 02.07.2021
ULY CLINIC. Ngozi kuwasha. https://www.ulyclinic.com/kuwashwa-ngozi. Imechukuliwa 02.07.2021
ULY CLINIC. Kuwawshwa pumbu na matibabu yake. https://www.ulyclinic.com/foramu/majadiliano-na-wataalamu/kuwashwa-sana-kwenye-pumbu-ni-dawa-gani-ya-kutumia. Imechukuliwa 02.07.2021
American family physician. Vaginitis. https://www.aafp.org/afp/2018/0301/p321.html. Imechukuliwa 02.07.2021
Mayo clinic. Lichen Sclerosis. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/lichen-sclerosus/diagnosis-treatment/drc-20374452. Imechukuliwa 02.07.2021
Medical news. What to know about pephigoid. https://www.medicalnewstoday.com/articles/318015. Imechukuliwa 02.07.2021
American Academy of dermatology asscociation. Howcan i treat genital soriasis. https://www.aad.org/public/diseases/psoriasis/treatment/genitals/genital-treat. Imechukuliwa 02.07.2021