Je, ni lini baada ya kutumia dawa za uzazi wa mpango nitazuia kupata mimba?
Baada ya kujifungua inachukua siku ngaoi dawa za uzazi wa mpango kunilinda kupata mimba?
Siku ya ngapi tangu kuanza dawa ya uzazi wa mpango itazuia mimba?
Kama ndo umetoka kujifungua, unaweza kuanza kutumia kidonge cha uzazi wa mpango chenye progestogen tu kati ya siku ya 1 hadi ya 21 baada ya kujifungua.
Ni wakati gani utakingwa na ujauzito ukianza dawa?
Dawa itakukinga na ujauzito ikitegejea na siku uliyoanza kutumia kama ifuatavyo
Kuanza kidonge siku ya 1 hadi 21
Ukianza dawa kati ya siku ya 1 hadi 21 baada ya kujifungua, dawa hii itakurinda mara moja dhidinya ujauzito unapoanza kumeza tu.
Kuanza dawa baada ya siku ya 21 ya kujifungua.
Kutumia dawa ya uzazi wa mpango yenye progesterone tu kuanzia siku ya 21 na iuendelea baada ya kujifungua itakuoinda kupata ujauzito baada ya kumeza dawa kwa siku 2.
Rejea za mada hii
Oral contraceprives. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK430882/. Imechukuliwa 17.04.2023
Hall KS, Trussell J, Schwarz EB. Progestin-only contraceptive pill use among women in the United States. Contraception. 2012 Dec;86(6):653-8. doi: 10.1016/j.contraception.2012.05.003. Epub 2012 Jun 6. PMID: 22682722; PMCID: PMC3440515.
Grimes DA, et al O'Brien PA, Raymond EG. Progestin-only pills for contraception. Cochrane Database Syst Rev. 2010:CD007541. [PubMed].
Sheth A, et al. A randomized, double-blind study of two combined and two progestogen-only oral contraceptives. Contraception. 1982;25:243–52. [PubMed].