Doxycycline ni dawa jamii ya antibayotiki inayotumika kutibu maradhi mbalimbali yanayosababishwa na bakteria.
Doxycycline ni dawa yenye nguvu na husababisha mvurugiko wa tumbo unaopelekea hali ya kuhisi kichefuchefu na kutapika.
Matumizi ya doxycycline wakati wa ujauzito huweza kuchochea hali ya kichefuchefu na kutapika, hata hivyo ikumbukwe kuwa, kichefuchefu na kutapika hutokea kwa wanawake wengi walio wajawazito na pia hali hizi zinaweza kusababishwa na sababu zingine zisizohusiana na ujauzito kama vile magonjwa ya mfumo wa tumbo n.k. Soma zaidi kuhusu visababishi vingine vya kichefuchefu na kutapikwa kwa mjamzito kwa kubofya hapa au soma makala ya kutapika sana wakati wa ujauzito
Licha ya kusaabisha kichefuchefu na kutapika, dawa hii huwa na maudhi mengine pia. Kusoma zaidi kuhusu maudhi mengine ya doxycycline bofya hapa.
Wasiliana na daktari wako siku zote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii.
Pia unaweza kuwasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa kubofya 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.
Makala zingine
Video ya kichefuchefu na kutapika nyongo kwa mjamzito