Je mtoto anaweza kuambukizwa virusi vya UKIMWi akiwa tumboni?
Wajawazito wenye maambukizi ya VVU na wakatumia dawa kwa kuzingatia maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa afya hupunguza hatari ya maambukizi kwa mtoto tumboni. Tafiti zinaonyesha kwamba kati ya wajawazito ellfu moja (1000) ni mmoja tu au chini yake huweza kupata maambukizi hayo katika kipindi chote cha kuwa tumboni, kuzaliwa au kunyonyesha.
Ukipata maambukizi mengine ya bakteria kwenye maji ya chupa ya uzazi au kufanyiwa kipimo cha kuchukua maji kwenye chupa hiyo huongeza hatari ya maambukizi. Hata hivyo watoto hupata maambukizi wakati wa kuzaliwa.
Je nikiwa situmi dawa naweza kuambukiza mtoto virusi vya UKIMWI?
Pasipo kutumia dawa za kufubaza maambukizi ya virusi vya UKIMWI, hali ya maambukizi kwa mtoto huwa kubwa zaidi. Tafiti zinaonyesha kuwa kati ya wajawazito 1000, wajawazito 150 hadi 450 huwaambukiza watoto wao endapo dawa za ARV hazikutumika. Maambukizi haya hutokea kabla na wakati wa kujifungua na wakati w akunyonyesha.
Wapi unaweza kupata maelekezo zaidi?
Maelekezo zaidi unaweza kupata kwenye makala za:
Rejea za mada hii:
Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. https://www.who.int/teams/global-hiv-hepatitis-and-stis-programmes/hiv/prevention/mother-to-child-transmission-of-hiv#. Imechukuliwa 24.06.2023
Diwan B, et al. HIV-2 and its role in conglutinated approach towards Acquired Immunodeficiency Syndrome (AIDS) Vaccine Development. Springerplus. 2013 Dec;2(1):7.
Nesheim SR, et al. Reconsidering the Number of Women With HIV Infection Who Give Birth Annually in the United States. Public Health Rep. 2018 Nov;133(6):637-643.
Peters H, Francis K, Sconza R, Horn A, S Peckham C, Tookey PA, Thorne C. UK Mother-to-Child HIV Transmission Rates Continue to Decline: 2012-2014. Clin Infect Dis. 2017 Feb 15;64(4):527-528.
Giroir BP. The Time Is Now to End the HIV Epidemic. Am J Public Health. 2020 Jan;110(1):22-24.
Mongelli M, et al. Estimating the date of confinement: ultrasonographic biometry versus certain menstrual dates. Am J Obstet Gynecol. 1996 Jan;174(1 Pt 1):278-81.
Tuomala RE, et al. Changes in total, CD4+, and CD8+ lymphocytes during pregnancy and 1 year postpartum in human immunodeficiency virus-infected women. The Women and Infants Transmission Study. Obstet Gynecol. 1997 Jun;89(6):967-74.