Swali la msingi
Habari daktari, je, kuna madhara ya kutumia p2 mara kwa mara, mfano mwezi uliopta nilitumia na mwezi nimetumia tena?
Majibu
Salama habari yako wewe! Asante kwa swali zuri sana.

Dawa P2 (Postinor 2) ni aina ya dawa ya dharura ya uzazi wa mpango inayofanya kazi kwa kuchelewesha au kuzuia yai kupevuka au kuungana na mbegu. Dawa hii imetengenezwa kwa homoni inayoitwa levonorgestrel.
Je, kuna madhara ya kutumia P2 mara kwa mara?
Ndiyo, matumizi ya mara kwa mara ya P2 hayashauriwi kwa sababu zifuatazo;
a. Huharibu mzunguko wa hedhi
Matumizi ya mara kwa mara yanaweza kufanya mzunguko wako wa hedhi usiwe wa kawaida unaoambatana na kuchelewa kwa hedhi, kutoka kabla ya muda, au kutokutoka kabisa.
b. Hupunguza ufanisi wa dawa
Dawa hii inaweza isifanye kazi vizuri ya kuzuia mimba kama inavyotegemewa ikitumia mara kwa mara na pia huwa haizuii mimba kwa asilimia 100.
c. Husababisha athari za kihomoni
Homoni levonorgestrel iliyo kwenye P2 inaweza kusababisha maudhi yafuatayo;
Kichefuchefu
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya matiti
Maumivu ya tumbo
Uchovu au mabadiliko ya kihisia
d. Haitoi ulinzi wa muda mrefu
P2 haizuii utungishaji wa mimba kwa muda mrefu, huzuia kwa tukio moja la ngono lililotokea kabla ya saa 72 (siku 3). Ukifanya tendo tena baada ya hapo, unaweza kupata mimba.
Ushauri
Ikiwa unajikuta unatumia P2 kila mwezi au mara kwa mara, ni vyema kutafuta njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu kama vile;
Vidonge vya uzaazi wa mpango
Sindano ya kila mwezi au ya kila baada ya miezi 3
Kijiti
Kitanzi (IUD)
Maoni yako
ULY CLINIC imefanya juhudi kukuelimisha, toa shukrani kwa kutoa maoni yako muhimu katika kuboresha makala zetu na kukupa maelezo au ushauri zaidi utakaokufaa. Maoni yako yatoe kwa kubofya hapa.
Rejea za mada hii;
World Health Organization. Emergency contraception: Fact sheet [Internet]. Geneva: WHO; 2022 [cited 2025 Apr 9]. Available from: https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/emergency-contraception
Trussell J, Raymond EG. Emergency contraception: A last chance to prevent unintended pregnancy. Contemporary OB/GYN [Internet]. 2013 [cited 2025 Apr 9];58(1):34–45. Available from: https://ec.princeton.edu/questions/ec-review.pdf
Cheng L, Che Y, Gülmezoglu AM. Interventions for emergency contraception. Cochrane Database Syst Rev. 2012 Aug 15;(8):CD001324. doi: 10.1002/14651858.CD001324.pub4.
Glasier A. Emergency postcoital contraception. N Engl J Med. 1997 Jul 17;337(15):1058–64. doi:10.1056/NEJM199710093371507
Kavanaugh ML, Jerman J. Contraceptive method use in the United States: trends and characteristics between 2008, 2012 and 2014. Contraception. 2018 Jan;97(1):14–21. doi:10.1016/j.contraception.2017.10.003
American College of Obstetricians and Gynecologists. Emergency contraception. Practice Bulletin No. 152. Obstet Gynecol. 2015 Sep;126(3):e1–e11. doi:10.1097/AOG.0000000000001045