Ukilinganisha na hali ya utulivu wa mwili, mazoezi huongeza mahitaji kwenye mwili kwa kiasi kikubwa. Wakati wa utulivu wa mwili mfumo wa neva wa utulivu (parasimpathetiki) hudumishwa. Mfumo huu hudhibiti upumuaji, mapigo ya moyo na shughuli mbalimbali za kimetaboliki.
Mazoezi huchochea mfumo wa neva wa simpathetiki unaopelekea kuamka kwa shughuli mbalimbali mwilini. Mwitikio huu hufanya kazi ya kusawazisha mahitaji ya mwili ili kukabiliana na ongezeko lilalosababishwa na mazoezi ambayo ni upumuaji, umetaboli, na mapigo ya moyo. Hivyo kazi zinazofanywa na mfumo huu wa simpathekiti ni kuongeza mapigo ya upumuaji, moyo na kuongeza umetaboli.
Jambo la mjadala
Magonjwa ya moyo bado yamekuwa mengi licha ya kufanyia kazi mikakati mbalimbali ya kinga na tiba. Vihatarishi vikuu vikiwa ni kuwa na kiwango kikubwa cha kolestro kwenye damu, shinikizo la juu la damu, kisukari, obeziti na matumizi ya mazao ya tumbaku. Vihatarishi hivi huchangia karibia asilimia 50 ya vifo kutokana na magonjwa ya moyo.
Kutofanya mazoezi huchangia kuongeza kupata vihatarishi hivyo wakati kufanya mazoezi huwa na matokeo ya kinyume yake.
Kutofanya mazoezi kunahusianishwa na obeziti, ambayo huweza ambatana na magonjwa mbalimbali. Obeziti mara nyingi hutokana na matumizi ya nishati nyingi zaidi ya mahitaji ya mwili.
Mambo mengine ya msingi kufahamu
Kuzingatia lishe pekee hupunguza uzito mara tatu zaidi ya mazoezi.
Dac Teoli1; Abhishek Bhardwaj2. Quality of life. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK536962/#:~:text=Definition%2FIntroduction,a%20specific%20point%20in%20time. Imechukuliwa 24.01.2023
Barofsky I. Can quality or quality-of-life be defined? Qual Life Res. 2012 May;21(4):625-31.
Singh S, et al. Quality of Life and its Relationship with Perceived Stigma among Opioid Use Disorder Patients: An Exploratory Study. Indian J Psychol Med. 2018 Nov-Dec;40(6):556-561.