Tumbaku ina kemikali nyingi zenye madhara kwenye chembe hai mwilini yanayosabisha magonjwa kadhaa na saratani. Baadhi ya kemikali mbaya zaidi kwenye tumbaku ni pamoja na nitrosamines, benzopyrine na hewa ya ukaa inayopatikana kwenye moshi wa zao hilin.k
Kuna zaidi ya kampaundi 2550 kwenye tumbaku na zaidi ya 4000 kwenye moshi wake.
Kampaundi ambazo ni hatari kwa afya ziko takribani 43 ambazo hupelekea saratani kama vile nikotiakune na nitrosamine na polonium 210.
Madhara ya tumbaku
Madhara ya utumiaji wa tumbaku katika makala hii yamegawanywa kutokana na sehemu inayoatiriwa na matumizi yake wakati wa ujauzito. Madhara hayo ni kama yalivyoainishwa hapa chini,.
Kwenye Moyo
Huyongeza hatari ya magonjwa ya mishipa ya damu na kuganda kwa damu. Wavutaji wa sigara huwa na hatari ya kupata mshituko wa moyo na kufa katika umri mmdogo kutokana na uvutaji wa sigara na m zao ya tumbaku.
Kisukari
Kisukari huongeza hatari ya kupata kisukari aina ya 2 kwa asilimia 30 hadi 40. Huweza kupelekea pia madhara yake kuonekana mapema zaidi au kuwa makali zaidi kama vile magonjwa ya figo na mzunguko hafifu wa damu.
Maambukizi
Uvutaji wa sigara hudhaifisha mfumo wa kinga mwilini na kufanya mtu kuata uwezekano wa kupata uambukizi wa bakteria na virusi.
Matatizo ya meno na kinywa
Uvutaji wa tumbaku huongeza hatari ya magonjwa ya kinywa, fizi na meno, ikiwa pamoja na kupoteza meno na ongezeko la hisia kwenye meno.
Kusinyaa kwa ubongo
Uvutaji wa tumbaku husababisha ubonfo kuzeeka mapema, hivyo kupelekea kupata magonjwa ya akili yanayotokana na uzee mapema kama ugonjwa wa alzheimers.
Kupoteza uwezo wa kunusa
Uvutaji wa sigara huharibu vinyweleo ndani ya mfumo wa hewa vinavyofanya kazi ya kuondoa uchafu katika mfumo huo ambao hupelekea upate hisia za harufu.
Magonjwa sugu
Uvutaji wa tumbaku huongeza hatari ya kupata magonjwa sugu ya mfumo wa hewa kama vile bronchaitiz, kusinyaa kwa mapafu, saratani ya mapafu, kinywa, njia ya hewa na figo na huchangua kusababisha saratani ya kongosho, tumbo, kizazi, ini, uume na puru.
Kupungua kwa kiwango cha oksijeni kwenye damu
Uvutaji wa sigara hujaza vijifuko vidogo vya mfumo wa hewa na hewa ya ukaa na kupelekea kukosa oksijeni. Hewa ya ukaboni ni sumu ambayo ikiingia kwenye damu hupunguza kiwango cha oksijeni.
Madhara ya tumbaku kabla ya wakati wa ujauzito
Kwanini uache uvitaji wa sigara kabla ya kuwa mjamzito?
Uvutaji wa sigara au tumbaku huambatana na mambo yafuatayo;
Huchangia kwa asilimia 20 ya watoto njiti wanaozaliwa
Huchangia asilimia 8 ya watoto wanaozaliwa kabla ya umri
Huchangia asilimia 5 ya vifo vya watoto wakati wa kuzaliwa
Rejea za mada hii:
Leading causes of death from tobacco smoking and benefits of stopping. Most smoking-related deaths arise from cancers (mainly lung cancer), respiratory disease (primarily chronic obstructive pulmonary disease – COPD), and cardiovascular disease (mostly coronary heart disease) (Action on Smoking and Health, 2016b).
More than 100 reasons to quit tobacco. WHO. https://www.who.int/news-room/spotlight/more-than-100-reasons-to-quit-tobacco? Imechukuliwa 04.12.24
Sherman CB. Health effects of cigarette smoking. Clin Chest Med. 1991 Dec;12(4):643-58. PMID: 1747984.
Terzikhan N, et al. Prevalence and incidence of COPD in smokers and non-smokers: the Rotterdam Study. Eur J Epidemiol. 2016 Aug;31(8):785-92. doi: 10.1007/s10654-016-0132-z. Epub 2016 Mar 5. PMID: 26946425; PMCID: PMC5005388.
Mishra S, et al. Tobacco: Its historical, cultural, oral, and periodontal health association. J Int Soc Prev Community Dent. 2013 Jan;3(1):12-8. doi: 10.4103/2231-0762.115708. PMID: 24478974; PMCID: PMC3894096.