Kutapika matapishi ya kijani au njano inayoelekea kijani ni kiashiria cha kutapika nyongo. Hii ni kawaida kutokea kwa watu wanaotapika sana bila kuweka kitu tumboni na ni hali ya kawaida ambayo haipaswi kumwogopesha mtu.
Wakati gani wa kuwa na hofu unapotapika nyongo?
Endapo unatapika nyongo pamoja na dalili zifuatazo unapaswa kutilia mashaka na kutafuta msaada wa daktari;
Kizunguzungu
Dalili za vidonda vua tumbo ( kiungulia, maumivu chembe ya moyo, maumivu wakati wa kula chakula n.k)
Kupumua kwa shinda
Kutapika nyongo kwa muda mrefu
Kutapika zaidi ya masaa 48 bila kupata nafuu
Kutapika kila kitu
Maumivu makali ya tumbo nay a ghafla
Kuwa na kisukari
Kuishiwa nguvu au kupata uchovu mkali
Kupata kizunguzungu au kuzimia
Maumivu makali ya kifua
Kutapika mara kwa mara katika mwaka
Damu kwenye matapishi au matapishi kuwa meusi au rangi ya unga wa kahawa
Maumivu makali ya kichwa na homa
Huduma ya kwanza kwa mtu anayetapika sana;
Hatua ya muhimu kuchukua endapo unatapika sana ni kufika hospitali ili kupatiwa matibabu kw akutundikiwa dripu, hii itasaidia rejesha kiwango cha madini na maji ulichopoteza.
Kama unatapika kwa kiasi na unaweza kunywa maji, fanya iwezekanavyo kunywa maji kiasi kidogo sana lakini mara kwa mara. Ukipata maji ya Oral au wengine huita ORS na hutumika kwa watoto wanaoharisha itasaidia kuwa kama huduma ya kwanza. Kengo ni kurejesha kiwango ulichopoteza kwa kutapika na kuzuia kupata shoku kutokana na kuishiwa maji mwilini.
Zuia kutumia vitu vinavyokuletea kichefuchefu kama vinywaji nyenye mafuta, sukari na viungo kwa wingi na vingine ambavyo vinaamsha kuchefuchefu chako.
Rejea za mda hii
Vomiting in adults. https://www.nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021
Catiele Antunes, et al. Upper Gastrointestinal Bleeding. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK470300/#: Imechukuliwa 28.06.2021
I.Dodd Wilson. Chapter 85Hematemesis, Melena, and Hematochezia. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK411/. Imechukuliwa 28.06.2021
Amyloidosis. my.clevelandclinic.org/health/diseases/15718-amyloidosis. Imechukuliwa 28.06.2021
Cyclic vomiting syndrome. niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/cyclic-vomiting-syndrome. Imechukuliwa 28.06.2021
Lamps LW, et al.Fungal infections of the gastrointestinal tract in the immunocompromised host: An update. DOI: 10.1097/PAP.0000000000000016. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff. Acute liver failure. mayoclinic.org/diseases-conditions/acute-liver-failure/symptoms-causes/syc-20352863. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff. Viral gastroenteritis (stomach flu). https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/viral-gastroenteritis/symptoms-causes/syc-20378847. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Food poisoning. mayoclinic.org/diseases-conditions/food-poisoning/symptoms-causes/syc-20356230. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Gastritis.mayoclinic.org/diseases-conditions/gastritis/symptoms-causes/syc-20355807. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Gastroesophageal reflux disease (GERD). mayoclinic.org/diseases-conditions/gerd/symptoms-causes/syc-20361940. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Intestinal obstruction. mayoclinic.org/diseases-conditions/intestinal-obstruction/symptoms-causes/syc-20351460. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Nausea and vomiting. mayoclinic.org/symptoms/nausea/basics/definition/sym-20050736. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Vomiting blood. mayoclinic.org/symptoms/vomiting-blood/basics/definition/sym-20050732
Nausea and vomiting in adults. nhs.uk/conditions/nausea-and-vomiting-in-adults/. Imechukuliwa 28.06.2021
Nausea and vomiting. my.clevelandclinic.org/health/symptoms/8106-nausea--vomiting. Imechukuliwa 28.06.2021
Vomit looks like coffee grounds after drinking alcohol. goaskalice.columbia.edu/answered-questions/vomit-looks-coffee-grounds-after-drinking-alcohol. Imechukuliwa 28.06.2021
Vomiting in adults. (2018). nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021