Kutapika njano au kupta matapishi ya njano au rangi ya chungwa hutokea masaa machache baada ya kupata ugonjwa ugonjwa unaosababisha kichefuchefu na kutapika. Rangi ya matapishi inaweza kuendelea kuwa njano endapo mtu atakula kitu kila anapotapika, au kubadilika na kuwa na rangi ya kijani, au njano inayoelekea kijani endapo mtu hali chochote baada ya kutapika. Rangi ya njano hutokana na majimaji ya chakula kilichomeng’enywa, hupaswi kuwa na woga unapotapika matapishi ya njano.
Visababishi vya kutapika njano
Kutapika njano huweza kusababishwa na;
Kula sumu ya chakula- dalili zinazoweza ambatani ni pamoja na maumivu ya tumbo, kuharisha na homa
Mafua ya tumbo- husababishwa na maambukizi ya virusitumboni kutokana na kula chakula au maji. Dalili zingine ni homa, maumivu ya misuli na tumbo
Mafua ya influenza- haya ni maambukizi ya virusi kwenye mfumo wa juu wa upumuaji, huleta dalili za kuchuruzika mafua na koo chungu kisha kuendelea kuwa na homa, maumivu ya misuli, uchovu maumivu ya kichwa na kutetemeka
Kipanda uso- huambatana na maumivu makali ya kichwa yanayoweza kudumu kwa masaa machache au siku kadhaa. Hisia za kutapika huweza kutokea na mtu hutapika kwa kujirudia rudia endapo maumivu ya kichwa yanaendelea
Ujauzito- huleta dalili ya kutapika wakati wa asubuhi, hutokana na mabadiliko ya homoni kipindi cha ujauzito.
Ugonjwa wa appendisaitiz
Homa ya mwendo
Matumizi ya dawa za kuua chembe zasaratani
Maambukizi sikio la kati
Matumizi ya dawa jamii fulani
Wakati gani wa kuwa na hofu unapotapika njano?
Endapo unatapika njano inayoambatana na dalili zifuatazo unapaswa kutilia mashaka na kutafuta msaada wa daktari;
Kizunguzungu
Kupumua kwa shinda
Kutapika nyongo kwa muda mrefu
Kutapika zaidi ya masaa 48 bila kupata nafuu
Kutapika kila kitu
Maumivu makali ya tumbo nay a ghafla
Kuwa na kisukari
Maumivu makali ya kifua
Kutapika mara kwa mara katika mwaka
Damu kwenye matapishi au matapishi kuwa meusi au rangi ya unga wa kahawa
Maumivu makali ya kichwa na homa
Kuishiwa nguvu au kupata uchovu mkali
Kupata kizunguzungu au kuzimia
Huduma ya kwanza kwa mtu anayetapika sana;
Hatua ya muhimu kuchukua endapo unatapika sana ni kufika hospitali ili kupatiwa matibabu kwa kutundikiwa dripu, hii itasaidia rejesha kiwango cha madini na maji ulichopoteza.
Kama unatapika kwa kiasi na unaweza kunywa maji, fanya iwezekanavyo kunywa maji kiasi kidogo sana lakini mara kwa mara. Ukipata maji ya Oral au wengine huita ORS na hutumika kwa watoto wanaoharisha itasaidia kuwa kama huduma ya kwanza. Kengo ni kurejesha kiwango ulichopoteza kwa kutapika na kuzuia kupata shoku kutokana na kuishiwa maji mwilini.
Zuia kutumia vitu vinavyokuletea kichefuchefu kama vinywaji nyenye mafuta, sukari na viungo kwa wingi na vingine ambavyo vinaamsha kuchefuchefu chako.
Rejea za mada hii
Vomiting in adults. https://www.nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021
Catiele Antunes, et al. Upper Gastrointestinal Bleeding. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK470300/#: Imechukuliwa 28.06.2021
I.Dodd Wilson. Chapter 85Hematemesis, Melena, and Hematochezia. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK411/. Imechukuliwa 28.06.2021
Amyloidosis. my.clevelandclinic.org/health/diseases/15718-amyloidosis. Imechukuliwa 28.06.2021
Cyclic vomiting syndrome. niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/cyclic-vomiting-syndrome. Imechukuliwa 28.06.2021
Lamps LW, et al.Fungal infections of the gastrointestinal tract in the immunocompromised host: An update. DOI: 10.1097/PAP.0000000000000016. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff. Acute liver failure. mayoclinic.org/diseases-conditions/acute-liver-failure/symptoms-causes/syc-20352863. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff. Viral gastroenteritis (stomach flu). https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/viral-gastroenteritis/symptoms-causes/syc-20378847. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Food poisoning. mayoclinic.org/diseases-conditions/food-poisoning/symptoms-causes/syc-20356230. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Gastritis.mayoclinic.org/diseases-conditions/gastritis/symptoms-causes/syc-20355807. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Gastroesophageal reflux disease (GERD). mayoclinic.org/diseases-conditions/gerd/symptoms-causes/syc-20361940. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Intestinal obstruction. mayoclinic.org/diseases-conditions/intestinal-obstruction/symptoms-causes/syc-20351460. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Nausea and vomiting. mayoclinic.org/symptoms/nausea/basics/definition/sym-20050736. Imechukuliwa 28.06.2021
Mayo Clinic Staff.Vomiting blood. mayoclinic.org/symptoms/vomiting-blood/basics/definition/sym-20050732
Nausea and vomiting in adults. nhs.uk/conditions/nausea-and-vomiting-in-adults/. Imechukuliwa 28.06.2021
Nausea and vomiting. my.clevelandclinic.org/health/symptoms/8106-nausea--vomiting. Imechukuliwa 28.06.2021
Vomit looks like coffee grounds after drinking alcohol. goaskalice.columbia.edu/answered-questions/vomit-looks-coffee-grounds-after-drinking-alcohol. Imechukuliwa 28.06.2021
Vomiting in adults. (2018). nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/vomiting-in-adults. Imechukuliwa 28.06.2021