Daktari: Naomba kuuliza, nina mimba ya wiki 38 napata maumivu makali sehemu za siri na kwenye nyonga, Je, ni dalili ya nini?
Hisia ya maumivu makali sehemu za siri kwa mjamzito zisizohusiana na kushiriki tendo zinaweza kutokana na mgandamizo wa mtoto kwenye mishipa ya fahamu ya maeneo ya nyonga, kitendo hichi hupelekea hisia za maumivu makali ama kuvutavuta kwenye uke, njia ya aja kubwa na maeneo mengine ambapo mishipa hiyo ya fahamu imesambaa kama sakafu ya nyonga na maeneo ya mapajani. Dalili hii hutokea sana kwenye ujauzito unaoelekea mwishoni yaani kuanzia wiki ya 37.
Ukiona dalili ya maumivu makali sehemu za siri kwa mjamzito ufanyaje?
Uonapo dalili hii, ili uweze kuitofautisha na dalili zingine, wasiliana na daktari wako kwa uchunguzi.
Je, kuna visababishi vingine vya maumivu makali sehemu za siri wakati wa ujauzito?
Ndio kuna sababu zingine zinaweza kusababisha maumivu haya ikiwa pamoja na maambukizi, na magonjwa mengine ya mishipa ya fahamu. Unahitaji kuwasiliana na daktari wako ili akuambie kama maumivu yako yanahusiana na ujauzito au la.