Makala hii imezungumzia kuhusu maumivu wakati wa kukojoa (Dysuria), Epidemiolojia, visabaishi, Dalili, wakati wa kumwona daktari, Uchunguzi, Matibabu na Kinga.
Maumivu wakati wa kukojoa (dysuria) ni dalili ya kawaida ambayo inaweza kutokana na hali mbalimbali za kiafya zinazoathiri mfumo wa mkojo.
Epidemiolojia ya dalili ya maumivu wakati wa kaukojoa

Maumivu wakati wa kukojoa ni tatizo linaloathiri watu wa rika zote, lakini linajitokeza zaidi kwa wanawake kutokana na muundo wa anatomia yao ambao huongeza hatari ya kupata maambukizi ya njia ya mkojo. Maambukizi ya njia ya mkojo ni miongoni mwa maambukizi ya bakteria yanayosababisha mzigo mkubwa kwa mifumo ya afya ulimwenguni.
Visababishi vya Maumivu wakati wa Kukojoa
Hali na magonjwa kadhaa yanaweza kusabaisha maumivu wakati wa kukojoa, miongoni mwazo ni kama ifuatavyo;
Maambukizi ya Njia ya Mkojo (UTI)
Bakteria kama Escherichia coli husababisha maambukizi kwenye kibofu cha mkojo au urethra, maambukizi haya hupelekea dalili ya maumivu wakati wa kukojoa.
Magonjwa ya Zinaa
Vimelea kama Neisseria gonorrhoeae na Chlamydia trachomatis vinaweza kuathiri mrija urethra na kusababisha maumivu wakati wote au wakati wa kukojoa.
Sindromu ya Urethra
Hali ambapo mtu anahisi maumivu kwenye njia ya mkojo bila sababu dhahiri ya kimatibabu.
Uvimbe wa Urethra
Kutokana na maambukizi, hasa yanayohusiana na magonjwa ya zinaa.
Dalili na Ishara zinazoambatana na maumivu wakati wa kukojoa
Zifuatazo ni dalili na ishara zinazoambatana na maumivu wakati wa kukojoa;
Hamu ya kukojoa mara kwa mara (frequency).
Maumivu au hisia ya kuwaka wakati wa kukojoa.
Maumivu ya chini ya tumbo (suprapubic pain).
Mkojo wenye damu (hematuria).
Homa na maumivu ya mgongo ikiwa maambukizi yameenea hadi kwenye figo.
Wakati gani wa kumwona daktari unapokuwa na maumivu wakati wa kukojoa?
Unapaswa kumwona daktari ikiwa hali na dalili zifuatazo zitaambatana na maumivu wakati wa kukojoa:
Dalili kali au zinazodumu
Maumivu makali au yanayozidi kuongezeka.
Dalili zinazodumu kwa zaidi ya siku mbili bila kupungua.
Kukojoa mkojo usio wa kawaida
Mkojo wenye damu
Mkojo wenye rangi isiyo ya kawaida au harufu mbaya kali.
Uchafu wa njano au kijani unaotoka kwenye tundu la mkojo
Dalili za maambukizi makali
Hisia za homa kali au baridi kali na kutetemeka
Maumivu ya mgongo au kiuno, hasa karibu na figo.
Kichefuchefu au kutapika.
Dalili za Magonjwa ya Zinaa
Maumivu wakati wa ngono.
Vidonda au uvimbe kwenye sehemu za siri.
Una hatari kubwa ya kupata maambukizi
Mambo yafuatayo yanaongeza hatari ya kupata maambukizi ambayo yakiambatana na maumivu wakati wa kukojoa ni lazima kutafuta msaada wa daktari:
Kuwa mjamzito.
Ikiwa una mfumo wa kinga dhaifu(upungufu wa kinga mwilini), kwa mfano, kutokana na ugonjwa wa kisukari, VVU/UKIMWI.
Ikiwa unatumia dawa za kuzuia mfumo wa kinga
Uchunguzi wa kitiba wa maumivu wakati wa kukojoa
Uchunguzi huhusisha mambo yafuatayo na vipimo;
Kuchukua historia ya mgonjwa na uchunguzi wa kimwili
Daktari atauliza kuhusu mwanzo wa dalili, historia ya kingono, na uwepo wa dalili nyinginezo.
Vipimo vya maabra
Vipimo hivyo huhusisha
Kuangalia uwepo wa bakteria, damu, au seli nyeupe za damu.
Kuotesha bakteria wa kwenye mkojo kwa utambuzi wa bakteria.
Nucleic Acid Amplification Tests kwa uchunguzi wa magonjwa ya zinaa.
Matibabu ya maumivu wakati wa kukojoa
Maumivu wakati wa kukojoa hutibiwa kwa kutegemea kisababishi, baadhi ya matibabu hayo huhusisha;
Matibabu ya maambukizi ya njia ya mkojo
Matumizi ya antibiotiki kama nitrofurantoin au ciprofloxacin kulingana na vimelea vilivyoonekana kwenye vipimo
Matibabu ya magonjwa ya zinaa
Dawa maalum kulingana na ugonjwa uliotambuliwa, kama azithromycin, ceftriaxone n.k
Matibabu ya sindromu ya Urethra
Matumizi ya dawa za kudhibiti dalili na mabadiliko ya mtindo wa maisha.
Njia za Kuzuia maumivu wakati wa kukojoa
Njia zifuatazo zinaweza kuzuia au kukinga dhidi ya dalili ya maumivu wakati wa kukojoa;
Kudumisha usafi wa kibinafsi.
Kunywa maji mengi ili kusaidia kutoa bakteria mwilini.
Kufanya ngono salama kwa kutumia kinga.
Kwa wale wenye UTIs zinazorudiarudia, daktari anaweza kupendekeza antibiotiki za kinga.
Rejea za mada hii
Brooks D, et al. Pathogenesis of the urethral syndrome in women and its diagnosis in general practice. Lancet. 1972;2:893–98.
Buchsbaum HJ, Schmidt JD, eds. Gynecologic and obstetric urology. Philadelphia: W.B. Saunders, 1982;538–39.
Carlton CE Jr, et al. Initial evaluation, including history, physical examination and urinalysis. In: Walsh PC, Gittes RF, Perlmutter AD, Stamey TA, eds. Campbell's urology. Philadelphia: W.B. Saunders, 1986;276–79.
Gillenwater JY, Harrison RB, Kynin CM. Natural history of bacteriuria in schoolgirls. N Engl J Med. 1979;301:396–99.
Kanaroff AL, et al. Management strategies for urinary and vaginal infections. Arch Intern Med. 1978;138:1069–73.
Komaroff AL. Acute dysuria in women. N Engl J Med. 1984;310:368–75.
Kraft JK, et al. The natural history of symptomatic recurrent bacteruremia in women. Medicine. 1977;56:55–60.
Meaves EM Jr. Prostatitis. Ann Rev Med. 1979;30:279–88.
Perez-Stable EJ. Urethritis in men. West J Med. 1983;138:426–29.
Smith DR. Symptoms of disorders of the genitourinary tract and effects of the psyche on renal and vesical function. In: General urology. Los Altos, CA: Lange Medical Publications, 1984;32–33, 631–37.