Metronidazole ni dawa ya antibiotiki inaotumika kutibu magonjwa yanayosababishwa na bakteria wanaouliwa na dawa hii: Baadhi ya magonjwa hayo ni:
Maambukizi ya bakteria wa anaerobiki ( Haswa katika vidondo)
Magonjwa ya zinaa (Huchanganywa na dawa zingine)
Vaginosis ya bakteria
Maambukizi baada ya upasuaji wa utumbo mpana
Maambukizi ya trikomoniasisi
Ugonjwa wa amoeba
Maambukizi ya gardinela
Maambukizi ya vimelea wa vidonda vya tumbo (Helikobakter pairoli). Hutumika na dawa zingine
Michomokinga kwenye mrija wa urethra isiyosababishwa na kisonono
Magonjwa ya michomokinga ndani ya ogani za nyonga kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa
Ugonjwa wa tumbo wa Crohn's
Vimelea gani huuliwa na metronidazole?
Ingawa vimelea hutengeneza usugu kwenye dawa hivyo kutoweza kuuliwa na dawa ambayo awali ilikuwa ikifanya hivyo, vimelea wafuatao hufahamika kuuliwa na dawa hii.
Vimelea jamii ya protozoa
Entamoeba histolytica
Giardia lamblia
Trichomonas vaginalis
Gardnerella vaginalis
Blastocysts
Balantidium coli
Vimelea jamii ya bakteria
Spishi za Peptostreptococci
Spishi za Clostridia spp
Bacteroides
Fusobacterium
Helikobacter pyroli
Clostridium difficile
Wapi utapata malezo zaidi kuhusu metronidazole
Pata maelezo zaidi katika makala za
Rejea za mada
Edwards DI. Nitroimidazole drugs--action and resistance mechanisms. I. Mechanisms of action. J Antimicrob Chemother. 1993 Jan;31(1):9-20.
Edwards DI. Reduction of nitroimidazoles in vitro and DNA damage. Biochem Pharmacol. 1986 Jan 01;35(1):53-8.
Löfmark S, Edlund C, Nord CE. Metronidazole is still the drug of choice for treatment of anaerobic infections. Clin Infect Dis. 2010 Jan 01;50 Suppl 1:S16-23.
NCBI. Metronidazole. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/9360057/#: Imechukuliwa 15.10.2024
Nix DE, Tyrrell R, Müller M. Pharmacodynamics of metronidazole determined by a time-kill assay for Trichomonas vaginalis. Antimicrob Agents Chemother. 1995 Aug;39(8):1848-52.
Pankuch GA, Jacobs MR, Appelbaum PC. Susceptibilities of 428 gram-positive and -negative anaerobic bacteria to Bay y3118 compared with their susceptibilities to ciprofloxacin, clindamycin, metronidazole, piperacillin, piperacillin-tazobactam, and cefoxitin. Antimicrob Agents Chemother. 1993 Aug;37(8):1649-54.
Ravdin JI, Skilogiannis J. In vitro susceptibilities of Entamoeba histolytica to azithromycin, CP-63,956, erythromycin, and metronidazole. Antimicrob Agents Chemother. 1989 Jun;33(6):960-2.
Ralph ED, Kirby WM. Unique bactericidal action of metronidazole against Bacteroides fragilis and Clostridium perfringens. Antimicrob Agents Chemother. 1975 Oct;8(4):409-14.