Visababishi vya vikanyagio vya miguu kuwaka moto
Kuna visababishi mbalimbali vinavyoweza kusababisha miguu kuwaka moto vikiwemo pamoja na
Upungufu wa virutubisho muhimu mwilini
Upungufu wa virutubisho husababisha uharibifu wa mishipa ya neva, na kupelekea mtu kuhisi miguu kuwa ya moto. Vitamin hizi huweza kuwa pamoja na vitamin folate, vitamin B6 na vitamin B12. Vitamin huwa na umuhimu katika mishipa ya fahamu kusafilisha taarifa sahihi. Kujua kazi zingine bonyeza hapa.
Baadhi ya mambo yanayoweza kusababisha upungufu wa vitamin ni, unyaji wa pombe wa kupindukia, magonjwa ya kula, kipato cha chini, uzee, ujauzito na upweke
Kisukari huharibu mishipa ya fahamu ya miguu, mishipa hii inapoharibiwa na sukari hushindwa kufanya kazi vizuri za akusafilisha taarifa za hisia. Tafiti zinaonyesha kuwa kisukari huongoza katika kuwa kisababishi cha miguu kuwaka moto. Dalili zingine mtu anaweza kuzipata akiwa na uharibifu wa mishipa ya fahamu kutokana na kisukari ni maumivu ya miguu, miguu kuchomachoma, na vidole kufa ganzi inawezekana zikatokea kwenye miguu au mikono lakini mara nyingi ni kwenye miguu.
Ujauzito
Mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito huweza kuambatana na tatizo la kuhisi miguu inawaka moto. Mbali na hili uzito wa mwili unavyoongezeka, huongeza miguu kugandamizwa kwa uzito na kuleta tatizo la kuhisi miguu ya moto.
Komahedhi
Mwanamke anapofikia komahedhi, mabadiliko mbalimbali ya mwili hutokea, mabadiliko haya huwa yale ya kuvurugika kwa mfumo wa homoni za uzazi (estrogen na progesterone). Mabadiliko haya husababisha madhara mbalimbali ikiwemo la mwanamke kuhisi miguu inawaka moto n.k. Komahedhi huanza kuanzia umri wa miaka 45 au 55 na kuendelea.