Majibu
Kukojoa mara kwa mara ni hali ya kuhisi haja ya kwenda kukojoa zaidi ya kawaida yako, unaweza kuwa unakojoa kiwango kikubwa cha mkojo kuliko kawaida ama kiasi kidogo kidogo sana.
Kukojoa mara kwa mara kunaweza kutokea wakati wa mchana au usiku tu au wakai wote yaani usiku na mchana.
Kukojoa mara kwa mara huweza kuasili hali ya usingizi, kazi ama utu wako.
Visababishi ni nini?
Kukojoa mara kwa mara huweza kusababishwa na magonjwa yanayoathiri mfumo wa mkojo kwenye sehemu yoyote ile. Mfumo wa mkojo huhusisha figo, mirija ya mkojo, kutoka kwwenye figo mpaka kwenye kibofu, kibofu cha mkojo, na mrija unaotoa mkojo nje ya mwili(urethra)