Swali hili nimeulizwa swali hili facebook na mwana dada
Majibu yangu yalikuwa yafuatayo;
Asee hili ni swali pana sana, naomba nambie unataka kujua kuhusu namna ya kumpa maziwa au? Kifupi kwa masuala ya chakula yeye anatakiwa kunyonya tu maziwa ya mama na asipewe chakula kingine au maji kwa sababu ya kinga zake za mwili kuwa chini, ukimpa chakula kingine unaweza sababisha akaanza ugua magonjwa ya tumbo kama tumbo kuuma na kuharisha. Pia mtoto huyu anatakiwa kunyonya angalau mara nane kwa siku, na kama inawezekana anyonye maranyingi iwezekanavyo ili kumfanya akue. Maziwa ya mama tu huwa na virutubisho ambavyo humsaidia kukua na pia huwa na kinga dhidi ya maradhi mbalimbali. Ukimnyonyesha mtoto vema utamfanya mtoto akue vema kiakili na kimwili. Mama pia anatakiwa kuzingatia kula vyakula bora ambavyo vinavirutubisho muhimu vya vitamin, protini, vyakula vyenye majimaji ya kutosha na vyakula vinavyoongeza kuzalisha maziwa. Mama anatakiwa kuepuka dawa ambazo zinaweza kumdhuru mtoto ambazo hupitia katika maziwa ya mama. Unaweza kusoma zaidi kuhusu vyakula vya kula wakati unanyonyesha mtoto au kuuliza swali na kujibiwa katika forumu hii