Kiwango cha chini cha damu ambacho mtu aliwahi ishi
Kiwango cha chini cha damu mwilini ambacho mgonjwa aliyekuwa amepewa dawa za usingizi kwa upasuaji na akaishi kimerekodiwa kuwa 0.6 (0.6g/dl.) Hiki ni kiwango cha chini zaidi ya kiwango ambacho kimewahi kurekodiwa duniani.
Kwa kiwango hichi cha chini zaidi, ni ngumu kwa mtu kuishi isipokuwa watu mtu huyo aliyeishi. Hii ni kutokana na madhara ya upungufu wa damu yanayoaambatana na kuferi kwa moyo kufanya kazi yake na hatimaye kifo.
Kiwango cha kawaida kwa wagonjwa mahututi anachoweza ishi nacho
Kwa kawaida, wataalamu wengi huongeza damu mgonjwa anapokuwa na damu chini ya 10g/dl, hata hivyo, tafiti nyingi zinaonyesha katika kiwango hicho, mwili bado unakuwa na uwezo wa kujihudumia pasipo madhara ya upungufu wa damu.
Kiwango cha chini kabisa mtu akiwa nacho na kushauriwa na wataalamu wengi duniani kwamba ni lazima mtu aongezewe damu ili aweze ishi ni 7g/dl.
Wagonjwa wengi wenye kiwango chini ya hicho hufariki dunia kutokana na upungufu wa damu mwilini.
Baadhi ya tafiti zilizohusisha mashahidi wa Yehova ambao kwa imani yao hawaongezewi damu, ilionekana kuwa wagonjwa wenye imani hii wengi walifariki dunia walipofikisha kiwango cha damu cha 5 au chini yake. Sababu ya awali ya kifo ni upungufu wa damu.
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi.
Kwa maelezo zaidi kuhusu kiwango cha kawaida cha damu, bofya hapa.
Kwa maelezo zaidi kuhusu upungufu wa damu mwilini bofya hapa.
Rejea za mada
Fakhry, S.M., Fata, P. How low is too low? Cardiac risks with anemia. Crit Care 8 (Suppl 2), S11 (2004). https://doi.org/10.1186/cc2845
Irita K, et al, [Present status of preparatory measures for massive hemorrhage and emergency blood transfusion in regional hospitals with an accredited department of anesthesiology in 2006] (article in Japanese). Masui. 2009;58:109–23.
Akaishi S, et al. Bood groups. In: Watanabe S, Kondo S, Matsunaga E, editors. In: Anthropological and Genetic Studies on the Japanese. Tokyo: University of Tokyo Press; 1975. pp. 77–107.
Nihon Kohden Corporation. MEK-6318J/K Celltac a Hematology Analyzer. Tokyo, Japan: Nihon Kohden Corporation; 2006.
Daniels G. Human Blood Groups. Oxford: Blackwell; 2002.
Dai J, et al. Case report: intraoperative management of extreme hemodilution in a patient with a severed axillary artery. Anesth Analg. 2010;111:1204–6.
Zollinger A, Hager P, Singer T, Friedl HP, Pasch T, Spahn DR. Extreme hemodilution due to massive blood loss in tumor surgery. Anesthesiology. 1997;87:985–7.
Orii R, et al. Peri-operative blood lactate levels in recipients of living-related liver transplantation. Transplantation. 2000;69:2124–7.