Je ikipia masaa 72 kabla ya kuanza kutumia PEP naweza kuzitumia?
Je ninaweza kutumia PEP baada ya masaa 72
Dawa za PEP zinaweza kutumika baada ya masaa 72?
Dawa za PEP zinaweza kutumi abaada ya siku 3?
Kuna njia zingine za kukinga kupata maambukizi ya VVU mtu aliyechelewa kuanza PEP ndani ya masaa 72?
top of page
To test this feature, visit your live site.
Muda wa PEP ukipita unafanyaje?
Muda wa PEP ukipita unafanyaje?
1 answer0 replies
Like
Maoni (1)
bottom of page
Kwa nini PEP huanzishwa ndani ya masaa 72
Maelezo haya yamelenga kujibu maswali yote yaliyoulizwa hapo juu kw akutumia ushahidi wa tafiti mbalimbali zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika.
PEP huanzishwa ndani ya masaa 24 hadi 72 toka mtu amehisi kuwa kwenye kihatarishi cha kupata maambukizi mfano;
Kuwa na ngono ya kulazimishwa au kubakwa na mtu asiyefahamika hali yake ya maambukizi
Kondomu kupasuka wakati unashiriki ngono na mwathirika wa VVU
Kujichoma na sindano au vitu vingine vya ncha kali vilivyotumia na wathirika wa VVU inaweza kuwa wakati wa kuhudumia mgonjwa au wakati wa upasuaji au kuchangia sindano ya dawa za kulevya na mwathirika n.k
Kwanini PEP itumike ndani ya masaa 24 hadi 72?
Tafiti zinaonyesha kuwa, inachukua masaa 72 kutambua uwepo wa Virusi vya UKIMWI kwenye tezi limfu, siku 5 kutambua uwepo wa virusi kwenye damu na takribani siku 8 kutambua uwepo kwenye maji ya uti wa mgongo. Tafiti hii inatoa dilisha la kuzuia kutokea kwa maambukizi kwa kuzuia virusi kusambaa, kuingia kwenye seli na kuzaliana. Hii ndo maana dawa hizi zinatolewa ndani ya masaa 72.
Je PEP inaweza kukukinga kupata maambukizi kwa asilimia 100%
Jibu ni ndio na hapana
Tafiti za wanyama zinaonyesha kuwa PEP endapo imeanzishwa ndani ya masaa 24 hadi 36, hukinga kwa asilimia 100 kuanza kwa maambukizi baada ya kutumia dozi kwa siku 28. Hata hivyo taarifa za binadamu zinaonyesha kuwa PEP haiwezi kukinga maambukizi kwa asilimia 100, hii inaweza kuchangiwa na mambo mbalimbali ambayo yameandikwa sehemu nyingine katika makala za ULY CLINIC. Hata hivyo, kuanza PEP ndani yamasaa 24 hadi 36,hukinga kupata maambukizi kwa zaidi ya asilimia 99.9
Matumizi ya PEP baada ya masaa 72 yanaweza kukukinga na maambukizi ya VVU
Tafiti zinaonyesha kuwa, baada ya masaa 72 kupita, virusi vya UKIMWI huwa vimeingia kwenye seli ulinzi mbalimbali mwilini kama ilivyoelezewa hapo juu, hivyo dawa za PEP haziwezi kuzuia tena maambukizi. Hata hivyo baadhi ya nchi haziruhusi kutolewa kwa PEP baada ya masaa 36 kwa kuwa umuhimu wake huwa ni mdogo, hii imeonekana kwenye baadhi ya tafiti kuwa nusu ya wanyama waliopewa dawa, waliata maambukizi hayo.
Endapo umechelewa kutumia ndani ya masaa 72 ufanyaje?
Endapo una moja ya kihatarishi cha kupata VVU na masaa 72 yamepita ndio umefahamu kuwa upo na kihatarishi, unapaswa kuonana na daktari kwa ushauri zaidi. Utakapokutana na daktari, utapewa ushauri nasaha kisha utapimwa. Utashauriwa pia endapo itawezekana kuja na chanzo cha hofu yako, mfano kama unahisi umeshiriki ngono na mwathirika, basi mwathirika huyo anabidi aje kupimwa pia kufahamu hali yake ya maambukizi kama anapatikana. Kama haiwezekani kupata chanzo basi utatakiwa kurudi tena baada ya mwezi mmoja kufanya kipimo kingine kuangalia kama una maambukizi.
Baada ya mwezi mmoja endapo utakutwa na maambukizi, utafanyiwa vipimo vingine na kuanzishiwa dalasa maalumu la ARV ili kufahamu mawili matatu kuhusu dawa hizo kisha kuanza kuzitumia endapo upo tayari. Kuanza kutumia dawa za ARV mapema husaidia kufanya mwili wako uwe imara na kudhibiti makali ya VVU.
Watu gani wapo hatarini kupata VVU licha ya kutumia PEP?
Tafiti zinaonyesha kuwa, watu katika makundi yafuatayo, licha ya kutumia PEP ndani ya masaa 72 wana hatari kubwa ya kupata maambukizi ya VVU
Wanaotumia sindano za kuchoma kwenye mishipa
Kuchomwa sindano ya damu ndani ya mishipa yenye VVU au kutoka kwenye damu ya mtu mwenye VVU
Rejea za maa hii
Advisory Committee for HIV and STD Prevention. HIV prevention through early detection and treatment of other sexually transmitted diseases-United States. Recommendations of the Advisory Committee for HIV and STD prevention. MMWR Recomm Rep 1998;47(RR-12):1–24. [PMID: 9701544] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/9701544. Imechukuliwa 19.06.2021
AIDSinfo. Recommendations for the Use of Antiretroviral Drugs in Pregnant Women with HIV Infection and Interventions to Reduce Perinatal HIV Transmission in the United States. 2017 Nov 14. https://aidsinfo.nih.gov/guidelines/html/3/perinatal/. Imechukuliwa 19.06.2021
Al-Hajjar SH , et al. Prevention of HIV-1 transmission with postexposure prophylaxis after inadvertent infected blood transfusion. AIDS 2014;28(10):1539–1541. [PMID: 24896805] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/24896805. Imechukuliwa 19.06.2021
Albert J, et al. Analysis of a rape case by direct sequencing of the human immunodeficiency virus type 1 pol and gag genes. J Virol 1994;68(9):5918–5924. [PMID: 7520096] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/7520096. Imechukuliwa 19.06.2021
American Academy of Pediatrics. Hepatitis B. 1997 Red Book: The Report of the Committee on Infectious Diseases. Elk Grove Village: American Academy of Pediatrics; 1997.
American Academy of Pediatrics. Issues related to human immunodeficiency virus transmission in schools, child care, medical settings, the home, and community. AmericanAcademy of Pediatrics. Committee of Pediatric AIDS and Committee on Infectious Diseases. Pediatrics 1999;104(2 Pt 1):318–324. [PMID: 10429018] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/10429018. Imechukuliwa 19.06.2021
American Academy of Pediatrics. Infant feeding and transmission of human immunodeficiency virus in the United States. Pediatrics 2013;131(2):391–396. [PMID: 23359577] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/23359577
Andreo SM, et al. HIV type 1 transmission by human bite. AIDS Res Hum Retroviruses 2004;20(4):349–350. [PMID: 15157352] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/15157352. Imechukuliwa 19.06.2021
Annandale D, et al. Raltegravir-based post-exposure prophylaxis (PEP): a safe, well-tolerated alternative regimen. J Int AIDS Soc 2012;15 (Suppl 4):18165.
Attia S, et al. Sexual transmission of HIV according to viral load and antiretroviral therapy: systematic review and meta-analysis. AIDS 2009;23(11):1397–1404. [PMID: 19381076] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/19381076. Imechukuliwa 19.06.2021
Auvert B, et al. Randomized, controlled intervention trial of male circumcision for reduction of HIV infection risk: the ANRS 1265 Trial. PLoS Med 2005;2(11):e298. [PMID: 16231970] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/16231970. Imechukuliwa 19.06.2021
Bader MS, et al. Postexposure prophylaxis for common infectious diseases. Am Fam Physician 2013;88(1):25–32. [PMID: 23939603] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/23939603. Imechukuliwa 19.06.2021
Baeten J, et al. Antiretroviral prophylaxis for HIV prevention in heterosexual men and women. N Engl J Med 2012;367(5):399–410. [PMID: 22784037] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/22784037. Imechukuliwa 19.06.2021
Bailey RC, et al. Male circumcision for HIV prevention in young men in Kisumu, Kenya: a randomised controlled trial. Lancet 2007;369(9562):643–656. [PMID: 17321310] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/17321310. Imechukuliwa 19.06.2021
Bartholomew CF, et al. Human bites: a rare risk factor for HIV transmission. AIDS 2006;20(4):631–632. [PMID: 16470132] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/16470132. Imechukuliwa 19.06.2021
Beasley RP, et al. Efficacy of hepatitis B immune globulin for prevention of perinatal transmission of the hepatitis B virus carrier state: final report of a randomized double-blind, placebo-controlled trial. Hepatology 1983;3(2):135–141. [PMID: 6339349] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/6339349. Imechukuliwa 19.06.2021
Beltrami EM, et al. Antiretroviral drug resistance in human immunodeficiency virus-infected source patients for occupational exposures to healthcare workers. Infect Control Hosp Epidemiol 2003;24(10):724–730. [PMID: 14587931] https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/14587931. Imechukuliwa 19.06.2021
HIV gov. Post-Exposure Prophylaxis https://www.hiv.gov/hiv-basics/hiv-prevention/using-hiv-medication-to-reduce-risk/post-exposure-prophylaxis. Imechukuliwa 19.06.2021