Swali la msingi
Habari za laoe daktair, nina mtoto wa mwaka na miezi3 anajoto sana nilimpeleka hospital akakutwa na joto39 akapimwa damu hana tatizo ni homa ya kawida akapewa paracetamol syrup na amoxicillin ya vidonge maana ana kikohozi kwa mbali sasa toka nimeanza kumpa dawa joto halishuki nachanganyikiwa leo siku ya 2.
Majibu

Pole sana kwa hali anayopitia mtoto wako, na naelewa unavyohisi kuchanganyikiwa—ni jambo la kawaida kwa mzazi kuona mtoto wake anaendelea kuumwa hata baada ya kuanza dawa.
Hapa kuna mambo muhimu ya kuzingatia;
Mambo ya kufuatilia kama joto halishuki
Ni kiasi gani cha joto kimepanda?
Kama bado linafika au kupita 39°C, ni vizuri kurudi hospitali haraka, hasa kama ni siku ya pili na hakuna mabadiliko.
Paracetamol anapewa kila baada ya saa ngapi?
Kwa kawaida, Paracetamol hutolewa kila baada ya saa 6 hadi 8 (sio zaidi ya mara 4 kwa siku), kulingana na uzito wa mtoto. Dawa isipotumiwa kwa muda sahihi, joto linaweza kushindwa kushuka.
Ana dalili zingine?
Hizi ni dalili za hatari na zinahitaji tiba ya dharura.
Kulia sana au kutulia sana
Kukataa kunyonya/kula
Kupumua kwa haraka au kwa shida
Kutapika kila kitu
Kuharisha kupita kiasi
Amoxicillin ni ya vidonge – Je, anaweza kumeza vizuri?
Mtoto wa mwaka 1 miezi 3 kwa kawaida hupewa Amoxicillin ya syrup. Kama ni vidonge, labda unazimenya au kuzivunja. Lakini kuna uwezekano hajameza dawa yote vizuri, na hii inaweza kufanya isifanye kazi ipasavyo.
Visababishi
Visababishi vya homa kwa mtoto wa mwaka mmoja na miezi 3 vinaweza kuwa vingi, na inategemea hali ya mtoto na dalili anazozionyesha. Hapa ni baadhi ya visababishi vya kawaida;
1. Maambukizi ya virusi (kama mafua, flu, COVID-19, RSV) – haya ndio chanzo kikuu cha homa.
2. Maambukizi ya bakteria:
Maambukizi ya masikio
UTI (maambukizi ya njia ya mkojo)
Nimonia( Homa ya mapafu)
Homa ya dengu (sehemu zenye mbu wengi)
2. Kuchomwa chanjo – homa hujitokeza kwa muda mfupi baada ya chanjo.
3. Kuchoka au kuota meno – mara chache sana husababisha joto juu ya 38.5°C.
4. Kuvuta hewa chafu (moshi wa sigara au vumbi)
5. Mazingira yenye joto kali sana au kuvaa sana
Matibabu ya nyumbani kwa mtoto mwenye homa
1. Dawa ya kushusha homa
Paracetamol (kulingana na uzito na umri)
Kwa mtoto wa mwaka 1 na miezi 3: kawaida ni 5ml ya 120mg/5ml paracetamol ya maji kila saa 6–8
Usimpe Ibuprofen bila ushauri wa daktari kwa mtoto chini ya miaka 2.
2. Mpe maji ya kutosha au maziwa ya mama
Husaidia kupunguza joto na kuzuia upungufu wa maji mwilini.
3. Mvike nguo nyepesi
Usimfunike nguo nyingi au sehemu kubwa ya mwili, hii huongeza joto.
Muweke sehemu yenye upepo au feni, lakini si baridi kali.
4. Tumia kitambaa kilicholowekwa maji ya uvuguvugu
Mpanguse kwenye kichwa, shingo, kwapani, makwapa, sehemu za siri na miguu.
Wakati wgani wa kumwona daktari haraka?
Muone daktari haraka sana kama mtoto ana;
Homa inaopita nyuzin joto 39°C na haishuki hata baada ya dawa
Anakataa kula/kunyonya kabisa
Anapumua kwa shida au kwa haraka
Anapoteza nguvu (amelegea, hataki kucheza, usingizi mwingi kupita kawaida)
Anatapika kila kitu
Ana degedege (mtoto anatetemeka au kuzimia ghafla)
Homa imeendelea zaidi ya siku 3
Anakohoa sana au ana harufu mbaya ya mdomo
Kuna vipele visivyoeleweka
Mkojo ni wa rangi ya ajabu au mkojo wa uchache sana
Rejea za mada hii:
World Health Organization. Pocket book of hospital care for children: guidelines for the management of common illnesses with limited resources. 2nd ed. Geneva: WHO Press; 2013.
American Academy of Pediatrics. Fever in Infants and Children. In: Hagan JF, Shaw JS, Duncan PM, editors. Bright Futures: Guidelines for Health Supervision of Infants, Children, and Adolescents. 4th ed. Elk Grove Village (IL): American Academy of Pediatrics; 2017. p. 470–475.
National Institute for Health and Care Excellence (NICE). Fever in under 5s: assessment and initial management (NICE guideline [NG143]). London: NICE; 2019 [cited 2025 Apr 16]. Available from: https://www.nice.org.uk/guidance/ng143. Imechukuliwa 18.04.2026
American Academy of Pediatrics. Managing Fever in Children. [Internet]. Itasca (IL): AAP; 2023 [cited 2025 Apr 16]. Available from: https://www.healthychildren.org/English/health-issues/conditions/fever/Pages/How-to-Take-a-Childs-Temperature.aspx. Imechukuliwa 18.04.2026
Centers for Disease Control and Prevention (CDC). Antibiotic Use in Children: What Parents Should Know. Atlanta (GA): CDC; 2022 [cited 2025 Apr 16]. Available from: https://www.cdc.gov/antibiotic-use/community/for-patients/children.html.Imechukuliwa 18.04.2026