Mzunguko wa hedhi umetengenezwa kwa muunganiko wa matukio tata yaliyopangiliwa yanayohusisha tezi haipothalamasi, pituitari ya mbele, ovari na ukuta wa ndani za kizazi ufahamikao kama endometriamu.
Mzunguko wa hedhi unaweza kuharibiwa kirahisi na sababu mbalimbali za kimazingira kama msongo, mazoezi makali, na uzito mkubwa kupita kiasi.
Mzunguko wa hedhi wa siku 28 hutokea kutokana na mwitikio wa mwili kwenye homoni zinazozalishwa na tezi zilizoorodheshwa hapo juu kama ifuatavyo;
Tezi haipothalamasi hutengeneza homoni gonadotropin zazi (GnRH), inayofanya kazi ya kuchochea pituitari ya mbele kuzalisha homoni follicle chochezi (FSH) na luteinizing (LH).
Kiwango na muda wa uzalishaji wa homoni gonadotropin huendana na kiwango cha homoni GnRH, mrejesho kutoka kwenye homoni jinsi za steroid, na mrejesho mwingine kwenye tezi zazi.
Homoni FSH na LH huchochea ovari kuzalisha homoni za jinsi ambazo ni estrogen na progesterone. Homoni hizi huchochea ukuaji wa ukuta wa ndani ya kizazi(endometria) na kudhuru pia ogani zingine mwilini.
Mrejesho wa uzalishaji wa estrogen na progesterone hutokea awali katika pituitari ya mbele, kupitia uzalishaji wa GnRH. Utengenezaji wa follicle, uovuleshaji, ukuaji wa endomeria, ushikiriaji wa ukuta wa endometria na ubomoaji wa ukuta endometriamu wakati wa mzunguko wa hedhi hutegemea mrejesho wa vichocheo vinavyozalishwa kwenye muhimili huu wa tezi haipothalamasi- pituitari ya mbele na Ovari
Mzunguko wa hedhi umegawanyika katika makundi mawili ya Ukuaji wa follicle na lutea kama unavyoakisiwa na mabadiliko katika ovari.
Siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi huelezewa kuwa ni siku ya kwanza ya kuona damu ya hedhi. Wakati huu wa mzunguko wa hedhi, endometriamu hubomolewa kutokana na uwepo wa kiwango cha chini cha estrojen. Hatua ya ukuaji wa ukuta wa endometria huelezewa kuwa ni muda kati ya kuona hedhi na uovuleshaji na huendana na kuongezeka kwa kiwango cha homoni estrojeni wakati kiwango cha progeterone huwa cha chini.
Kiwango cha estrojeni kinapoongezeka, ukuta wa endometria hunenepa na huambatana na kukua kwa tezi na mishipa ya damu ya ukuta huo.
Hatua ya utagaji wa yai ni muda kati ya yai linapotoka hadi hedhi nyingine inapotokea. Mara baada ya yai kuzalishwa, kiwango cha
progesterone huongezeka na kupelekea ongezeko la uzalishaji wa glycoge na ute kwa wingi na utayari kujiandaa kwa endometriamu kupokea kiinitete kilichochavushwa.
Katika hatua ya mwisho ya utagaji wa yai , kama mimba isipotokea na kiwango cha estrogen na progesterone hupungua na mishipa ya damu katika endometriamu husinyaa na kusababisha ukuta kukosa chakula na kubomoka hivyo kupelekea kuona damu ya hedhi ya kila mwezi.
Wastani wa siku katika mzunguko wa hedhi huwa siku 28, hii haimaanishi kuwa mzunguko wa hedhi huwa wa siku 28. Mzunguko wa hedhi unaweza kutofautiana kati ya mzunguko na mzunguko na kati ya mwanamke mmoja na mwingine.
kwa kuongezea, licha ya kuwa na utofauti baina ya mzunguko na mzunguko, urefu wa kipindi cha luteal na ukuaji wa folliko hutofautiana. Licha ya tafiti kuonyesha kuwa kipindi kinachoathiriwa ni cha ukuaji wa folliko, mabadiliko katika kipindi cha lutea pia hupaswa kuzingatiwa.
Wapi utapata maelezo zaidi?
Unaweza kupata maelezo zaidi katika makala zifuatazo. Bofya makala husika kusoma.
Rejea za mada hii
Anderson LD, Hirshfield AN. An overview of follicular development in the ovary: From embryo to the fertilized ovum in vitro. Maryland Medical Journal. 1992;41:614–620.Â
Byskov AG, et al. Embryology of mammalian gonads. In: Knobil E, Neill J, editors. The Physiology of Reproduction. Vol. 1. New York: Raven Press, Ltd.; 1994. pp. 487–540.
Dong J, et al. Growth differentiation factor-9 is required during early ovarian folliculogenesis. Nature. 1996;383:531–535. doi: 10.1038/383531a0.
Hirshfield AN. Development of follicles in the mammalian ovary. International Review of Cytology. 1991;124:43–101. doi: 10.1016/s0074-7696(08)61524-7.
Matzuk MM, et al. Intercellular communication in the mammalian ovary: oocytes carry the conversation. Science. 2002;296:2178–2180. doi: 10.1126/science.1071965.
Matzuk MM, Lamb DJ. Genetic dissection of mammalian fertility pathways. Nat Med. 2002;8(S1):S41–S49. doi: 10.1038/ncb-nm-fertilityS41.
Pangas SA, et al. Genetic models for transforming growth factor beta superfamily signaling in ovarian follicle development. Mol Cell Endocrinol. 2004;225:83–91. doi: 10.1016/j.mce.2004.02.017.
Rajkovic A, et al. NOBOX deficiency disrupts early folliculogenesis and oocyte-specific gene expression. Science. 2004;305:1157–1159. doi: 10.1126/science.1099755.Â
Speroff L,r et al. Clinical Gynecologic Endocrinology and Infertility. Lippincott Williams & Wilkins; 2005.
Suzumori N, et al. Nobox is a homeobox-encoding gene preferentially expressed in primordial and growing oocytes. Mech Dev. 2002;111:137–141. doi: 10.1016/s0925-4773(01)00620-7.