Makala hii imejibu namna ya kufahamu urefu wa mzunguko wa hedhi kwa ajili ya kufahamu siku ya hatari kushika mimba.
Swali la msingi

Hello dokta, pole na majukumu, samahani naomba kuuliza swali mwezi wa kumi na mbili 2024 nilipata hedhi tar 13/12, mwezi wa kwanza 2025, 11/1, mwez wa pili 13/2 na mwezi wa tatu 12/3, je, huu ni mzunguko wa siku ngapi?
Majibu
Ili kupata urefu wa mzunguko wako wa hedhi, tunahesabu idadi ya siku kati ya kila hedhi hadi nyingine:
Kutoka 13/12 hadi 11/1 → Siku 29
Kutoka 11/1 hadi 13/2 → Siku 33
Kutoka 13/2 hadi 12/3 → Siku 28
Kwa mujibu wa mahesabu haya, mzunguko wako wa hedhi hutofautiana kati ya siku 28 hadi 33. Mzunguko wa kawaida wa hedhi huwa kati ya siku 21 hadi 35, hivyo mzunguko wako bado upo ndani ya kiwango cha kawaida. Kama unataka wastani wa mzunguko wako, unapaswa kujumlisha siku zote kisha gawa kwa idadi ya mizunguko: Hivyo kwenye mzunguko wako uliotaja hapa mahesabu ni kama ifuatavyo;
(29+33+28)÷3= 30
Kwa hiyo, wastani wa mzunguko wako wa hedhi ni siku 30. Mzunguko huu wa wastani wa miezi mitatu ni mzuri kutumia kutabiri siku za hatari na kushika mimba.
Video za kutabiri siku za kushika mimba kwa mzunguko wa siku 30
Video ya jumla ya mahesabu ya siku ya kushika mimba mzunguko wa siku 30
VIdeo ua kushika mimba mwezi Aprili mzunguko wa siku 30
Video ya kushika mimba Mei 2025, mzunguko wa siku 30
Rejea za mada hii
Menopausal Transition. Obstetrics and Gynecology Clinics of North America, 38(3), 595–607. https://doi.org/10.1016/j.ogc.2011.05.011
Fehring, R. J., Schneider, M., & Raviele, K. (2006). Variability in the Phases of the Menstrual Cycle. Journal of Obstetric, Gynecologic & Neonatal Nursing, 35(3), 376–384. https://doi.org/10.1111/j.1552-6909.2006.00051.x
Treloar, A. E., Boynton, R. E., Behn, B. G., & Brown, B. W. (1967). Variation of the Human Menstrual Cycle Through Reproductive Life. International Journal of Fertility, 12(1), 77–126.
Chiazze, L., Brayer, F. T., Macisco, J. J., Parker, M. P., & Duffy, B. J. (1968). The Length and Variability of the Human Menstrual Cycle. JAMA, 203(6), 377–380. https://doi.org/10.1001/jama.1968.03140060001001
Cole, L. A. (2010). Menstrual Cycle Physiology: Reproductive Hormones. Clinical Chemistry, 56(6), e1–e4. https://doi.org/10.1373/clinchem.2010.144477