Ikiwa unatafuta kupata ujauzito haraka, kuna mambo muhimu ya kuzingatia ili kuongeza uwezekano wa kutunga mimba kwa haraka. Hapa kuna mwongozo wa hatua unazoweza kuchukua:
1. Fahamu Siku yako ya uovuleshaji

Siku ya uovuleshaji, yai hutolewa na kuwa tayari kutungishwa endapo utashiriki ngono siku 1 hadi 4 kabla au siku hiyo ya uovuleshaji. Unaweza kufahamu siku hiyo kwa kufanya mambo yafuatayo;
Hesabu mzunguko wako wa hedhi ambao kwa kawaida ni siku 21-35, na siku za hatari zaidi za kushika mimba ni kati ya siku ya 11 hadi 21 ikiwa una mzunguko wa siku 28.
Tumia kalenda ya uovuleshaji aukikokoteo cha uovuleshaji kusaidia kufuatilia siku zako za hatari.
Angalia ishara za mwili kama: Majimaji ya ukeni kuwa meupe na kunata kama yai bichi, kuongezeka kwa hamu ya tendo la ndoa na maumivu kidogo upande mmoja wa tumbo (Maumivu ya uovuleshaji).
2. Shiriki Tendo la Ndoa kwa Wakati Sahihi
Kufanya tendo la ndoa angalau mara 3-4 kwa wiki huongeza uwezekano wa kupata mimba haraka.
Kufanya tendo la ndoa kabla na wakati wa uovuleshaji (siku 2-3 kabla ya yai kuachiliwa) huongeza nafasi za mbegu kufanikisha urutubishaji.
Baada ya tendo la ndoa, kaa chini au lala chali kwa dakika 10-15Â ili kusaidia mbegu kusafiri vizuri kwenda kwenye kizazi.
3. Imarisha Afya Yako
Kunywa maji mengi ili kusaidia ute wa uzazi kuwa mzuri.
Epuka sigara, pombe, na kahawa nyingi kwani zinaweza kuathiri uzazi.
Fanya mazoezi mara kwa mara lakini usizidishe kwa sababu mazoezi kupita kiasi yanaweza kuathiri uovuleshaji.
Hakikisha unakula vyakula vyenye foliki asidi, madini ya chuma, na vitamini kwa wingi kama mboga za kijani, matunda, samaki, na nafaka zisizokobolewa.
4. Mwanaume pia anatakiwa kuwa na afya bora
Ajiepushe na joto kali kwenye sehemu za siri mfano: sauna au kuweka laptop kwenye mapaja.
Ale vyakula vyenye zinki na vitamini C kama mayai, nyama, karanga, na machungwa kusaidia mbegu kuwa zenye afya njema.
Apunguze msongo wa mawazo kwani unachangia kupunguza idadi ya mbegu.
5. Pata ushauri wa daktari
Unashauriwa kupataushauri wa daktari endapo;
Umekuwa ukijaribu kupata mimba kwa zaidi ya miezi 6-12Â bila mafanikio.
Una matatizo ya hedhi zisizo na mpangilio.
Una historia ya maambukizi ya kizazi au matatizo ya uzazi.
Hitimisho
Ukiwa makini na mzunguko wako wa hedhi, kushiriki tendo la ndoa kwa wakati sahihi, na kuzingatia afya yako na ya mwenza wako, unaweza kuongeza uwezekano wa kushika mimba haraka.