Hili ni swali niloulizwa leo na mgonjwa wangu kuhusu visababishi vya maumivu ya jicho, na nilimjibu kama ifuatavyo;Maumivu ya jicho ni ile hali inayotokea endapo kuna tatizo katika kuta za nje au ndani ya jicho. Kuwa na maumivu makalai ya jicho kunaweza kumaanisha kuna shuda kubwa kwenye jicho inayoweza kupelekea kupoteza kuona au kuwa una shida kubwa inayohitaji tiba ya haraka. Maumivu ya jicho huweza kuelezewa kama hali ya jicho kuwasha, kuungua, au ya kuchoma choma.Mara nyingi maumivu ya jicho hutokana an kuingia kwa kitu kigeni kwenye macho ambacho husabaisha kuamka kwa chembe hai za mwili ili kupambana na kumwondoa mgeni huyo, matokeo yake huwa ni uzalishaji wa kemikali zinazosababisha kuhisi maumivu na kubadilika kwa hali ya jicho ikiwa pamoja na rangi, kwa pamoja inaitwa michomo kwenye macho. Maumivu yanayotoka ndani ya jicho huwa na sifa za kuchoma au kuuma
Sababu zinazoweza kusababisha maumivu ya jicho huwa pamoja;
Aleji/Mzio na kitu fulani
Michomo ya kwenye kope
Kuziba kwa mrija wa machozi
kuota kwa kifuko cha maji kwenye macho
Maumivu ya kichwa
Matumizi ya lensi za kuvaa
Macho kuwa makavu
Kitu kigeni kwenye macho
Tatizo la glaukoma
Majera, au kujigonga kwenye macho au kuungua
Michomo kwenye sehemu ya jicho yenye rangi nyeupe
Michomo kwenye sehemu nyekundu ya konea
Michomo ya mshipa wa fahamu wa optic
Michomo kwenye kuta ya konjuctiva
Michomo kwenye ukuta w akatikati wa macho
Uvimbe mwekundu unauuma iliyo karibu na kingo za kope ya jicho
Kugeuza kope kwa ndani au nje kwa nje
Unamaumivu ya jicho? Kutana na daktari wako kwa tiba au tumia application ya uly clinic kupata tiba na daktari wako