top of page
To test this feature, visit your live site.
Ni yapi matumizi sahihi ya barakoa kuzuia maambukizi ya COVID 19 au Corona?
Ni yapi matumizi sahihi ya barakoa kuzuia maambukizi ya COVID 19 au Corona?
1 answer0 replies
Like
Maoni (1)
bottom of page
Barakoa nzuri ni ipi?
Barakoa nzuri ni ile yenye uwezo wa
· Kufunika vema pande zote za mdomo na pua lakini kukuachia uhuru wa kupumua
· Kushikizwa kwa Kamba au barabendi inayopita nyuma ya sikio au nyumaya kichwa
· Iwe na Zaidi ya kuta moja ya kitambaa au fabriki
· Isizuie upumuaji wako
· Iwe na uwezo wa kusafishwa/kufuliwa na kupigwa pasi bila kuharibika
Inashauriwa na shirika la kimataifa la kupambana na kuzuia magonjwa CDC kuwa, endapo itashindikana kuzuia kujichanganya kwenye mkusanyiko wa watu kama maeneo ya kulia chakula, sokoni, dukani n.k ni vema ukavaa barakoa ya nguo ili kuzuia maambukizi ya corona.
Namna gani ya kuvua barakoa yako
Vua barakoa kwa kushika Kamba nyuma ya sikio, usishike barakoa sehemu ya mbele maana inauwezekano mkubwa wa kuwa na maambukizi. Eneo hili la mbele ndipo hewa chafu, bakteria na virusi wanaweza kuwepo kutoka kwenye hewa, hivyo eneo hili si salama. Shika Kamba nyuma ya sikio kuvua barakoa yako na kisha itupie kwenye ndoo ya maji yenye sabuni au deto na ikae kwa muda wa masaa mawili kabla ya kuifua.
Unatakiwa kubadilisha barakoa mara ngapi kwa siku?
Badilisha barakoa kila mara utakapotaka
· Kula chakula
· Kunywa maji
· Kunywa chai
Kwa kifupi kila utakapotaka kuingiza kitu kinywani ni lazima uvae barakoa mpya. Hii ni kwa sababu kurudia barakoa ile ile inakuweka hatarini kupata maambukizi.
Unatakiwa kuwa na barakoa ngapi?
ULY clinic inashauri uwe na wastani wa barakoa tatu, barakoa ya kwanza itavaliwa wakati unataka kutoka nje kwenda kutafuta mahitaji yako. Unaporejea nyumbani kabla hujaingia ndani vua barakoa kama ilivyoelekezwa hapo juu kwa kushika Kamba iliyo nyuma ya sikio na kisha kuitupa katika chombo maalumu cha kutunzia uchafu. Endapo barakoa yako ni ya kufua, iweke kwenye ndoo ya maji yenye sabuni au deto ambayo utakuwa tayari ulishaiandaa na ipo nje ya nyumba. Funika ndoo na kisha jitakase kwa kunawa mikono yako kwa sabuni na maji tiririka au kwa kutumia vitakasa mikono. Hapa unaweza kufungua mlango na kuingia ndani ya nyumba yako. Unapoingia ndani usiguze chochote wala usiingie na viatu. Elekea bafuni badilisha nguo na oga. Ukimaliza kuoga unaweza kurejea sebleni na kukaa Pamoja na familia yako. Endapo umekuja na vitu kutoka ofisini hakikisha unavifuta maeneo ya juu kwa kitambaa safi kilichochovywa kwenye spiriti au kitakasa mikono. Hii inategemea aina ya vitu ulivyokuja navyo kwani baadhi vinawez akuharibika endapo vitasafishwa kwa vitakasa.
Kwa watu ambao wapo wanaenda makazini, unapoamka na kwenda kazini vaa barakoa yako ya nguo mara unapoondoka nyumbani kwenda ofisini na haikisha unabeba barakoa zingine mbili kwenda nazo. Unapofika ofisini na kufanya shughuli zako hakikisha hushiki barakoa yako sehemu ya mbele. Rekebisha barakoa yako endapo haijakaa vizuri kwa kushika Kamba nyuma ya sikio. Unapotaka kwenda kupata kifungua kinywa, vua barakoa hiyo na kuiweka kwenye ndoo yenye majiya sabuni. Unapomaliza kifungua kinywa vaa barakoa safi, fanya hivi kila unapotaka kula chakula au kunywa maji endapo utakuwa maeneo yenye msongamano wa watu. Hakikisha baada ya masaa mawili unafua barakoa uliyoloweka kwenye ndoo na kuianika kabla ya kuzirudia kuvaa tena.
Soma zaidi kwa kubonyeza hapa