Kutofika kileleni imekuwa changamoto kubwa kwa wanawake wengi. Idadi ya wanawake wanaotafuta ushauri na matibabu mtandaoni kutokana na kutofika kileleni imekuwa ikiongezeka kila siku. ULY CLINIC tunaUnaweza kufanya mambo yafuatayo ili kufika kileleni kwa mwanamke.
Uwazi
Kuwa muwazi kwa mpenzi wako kuhusu suala la kufika kileleni, ongea naye kuhusu unavyojihisi vema ukifika na endapo unaebwa na mawazo wakati wa tendo kwa sababu ya mawazo ya kutofika, kuwa muwazi ili msaidiane kufika.
Vilainishi
Tumia vilainishi kusaidia kulainisha maeneo ya uke, hii ni njema kwa mwanamke ambaye hana ute wa kutosha au anayeishiwa ute wakati wa tendo.
Kuwaza wakati mzuri wa tendo
Muda mfupi kabla na wakati wa kujamiana hakikisha akili yako inawaza kuhusu tendo na namna unavyosisimuka ukiguswa kwenye aeneo muhimu kwako. Kufanya hivyo mwili wako hujiandaa kwa kutoa homoni zinazoweza kukusaidia kufika kileleni.
Jisisimue kwa njia mbalimbali wakati wa kujamiana kama vile matumizi ya vidole, ulimi na busu la kina.
Ngono ya kistaarabu
Shauriana na mwenza wako kufaya mapenzi taratibu, kufanya hivyo huweza kusisimua mwili wako kwa muda mrefu na kuongeza uwezekano wa kufika kileleni mara nyingi. Wanaume wengi hudhania kuwa ngono ya harakaharaka na kutumia nguvu nyingi huwafurahisha wanawake lakini ni kinyume chake kwa wanawake wengi. Mishipa ya fahamu ya maeneo ya uke inapaswa kusisimuliwa taratibu na haswa kwenye kinembe kwa muda mrefu, kasi ya kusisimua inaongezeka kwa jinsi utakavyomwambia mpenzi wako aongeze unapohisi utamu unaongezeka zaidi.
Pata vipimo
Kwa baadhi ya wanawake wanahitaji kuonana na daktari kwa vipimo vya kuchunguza mwili kama kuna magonjwa yoyote au hali ya kianatomia inayoweza kuchangia tatizo la kutofika kileleni. Utafanyiwa vipimo kulingana na kinachodhaniwa kuwa kisababishi kwako baada ya mazungumzo ya kitaalamu.
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi
Wasiliana na daktari wako kwa maelezo zaidi. Unaweza kupata maelezo zaidi pia kuhusu mwanamke kufika kileleni katika makala ya dawa ya mwanamke kufika kileleni.
Rejea za mada hii
Uptodate. Treatment of female orgasmic disorder. https://www.uptodate.com/contents/treatment-of-female-orgasmic-disorder
NIHS. https://www.nhs.uk/common-health-questions/sexual-health/what-is-an-orgasm/. Imechukuliwa 13.11.2024
ULY CLINIC. Dawa ya mwanamke kufika killeni. https://www.ulyclinic.com/post/dawa-ya-kufika-kileleni-ke-ulyclinic. Imechukuliwa 13.11.2024