Swali lililoulizwa ni, Je, mtu akiwa na nimonia ni kwamba ana ukimwi?
Majibu.
Si kweli UKIMWI hutambulika kwa kupima tu. Watu wazima na watoto wenye kinga dhaifu ya mwili huweza shambuliwa na vimelea mbalimbali wanaosababisha maradhi mbalimbali ikiwa pamoja na nimonia. Baadhi ya haki na magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili yameorodheshwa hapa chini.
Hali na magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili
Baadhi ya hali na magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili ni:
Matumizi ya dawa zinazoshusha kinga ya mwili kama dawa jamii ya corticosteroid, dawa za kuua chembe za saratani
Saratani ya chembe za mfumo wa kinga ya mwili
Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi
Lishe duni(utapiamlo, kifadulo n.k)
Kwa maelezo zaidi waweza kusoma makala ya kushuka kwa kinga ya mwili kutokana na magonjwa mengine